24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

AJIB, NGOMA WABEBESHWA MAJUKUMU MAZITO YANGA

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amepanga kuunda kombinesheni mpya ikiwahusisha mastraika Ibrahim Ajib na Donald Ngoma.

Lwandamina anaamini Ajib ambaye ametua Yanga kipindi hiki cha usajili wa msimu ujao kwa mkataba wa miaka miwili na Ngoma watakuwa moto wa kuotea mbali, kama atawapanga pamoja kuanzia katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Yanga itaikabili Simba katika pambano la Ngao ya Jamii litakalopigwa Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ajib amekuwa akijifua vikali na kikosi hicho cha Jangwani kilichopo kambini mkoani Morogoro, wakati Ngoma alitarajiwa kuwasili jana akitokea nchini kwake Zimbabwe tayari kujiunga na timu hiyo kwa maandalizi ya msimu mpya.

Lwandamina aliliambia MTANZANIA jana kuwa, anatarajia mambo makubwa kutoka kwa Ajib, hivyo ameanza kumtengeneza ili awe fiti zaidi huku akimsubiri Ngoma.

“Nimepanga kumtumia kwenye kikosi changu cha kwanza kwa sababu hiyo nimekuwa nikimfanyisha mazoezi binafsi tangu tulipokuja huku kambini Morogoro.

“Ni mchezaji mwenye kipaji lakini anatakiwa kuwa fiti zaidi ndiyo maana nimeamua kumpa mazoezi binafsi, naamini akicheza na Ngoma kutakuwa na kitu kizuri,” alisema Lwandamina.

“Matarajio yangu mpaka tutakapocheza mechi ya Ngao ya Jamii watakuwa tayari wameelewana na kutoa matokeo chanya.”

Mzambia huyo alisema kwa sasa bado hajapata kikosi cha kwanza, huku akisisitiza kwa kuwataka wachezaji wake kujituma katika mazoezi ili kumshawishi.

Lwandamina msimu uliopita aliwapa jukumu la kusimama kama washambuliaji wa mbele, Amisi Tambwe na Obrey Chirwa ambao walionekana kuleta tija kutokana na kila mmoja kufunga mabao ya kutosha.

Tambw hadi msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara  unamalizika, alikuwa amefanikiwa kufunga mabao 11 wakati Chirwa alifunga mabao 12 na Ngoma nane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles