24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

AJIB, KICHUYA WAPEWA KAZI MAALUMU

Na WINFRIDA MTOI-Dar es Salaam


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amewapa kazi maalumu wachezaji, Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib ya kuhakikisha wanaendeleza makali yao katika michuano ya Chalenji ili kuipa ubingwa Kilimanjaro Stars.

Ajibu na Kichuya ni miongoni mwa wachezaji 23 wanaounda  kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoondoka jana kwa ndege kwenda  Kenya, kushiriki michuano ya Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Desemba 3, mwaka huu.

Katika michuano hiyo, Kilimanjaro Stars itakata utepe kwa kumenyana na Libya.

Akizungumza katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili ya kuiaga timu hiyo, Mwakyembe alisema ana matumaini makubwa Kilimanjaro Stars itarejea na ubingwa kutokana na  ubora wa wachezaji wanaounda kikosi hicho.

Alisema anafahamu  Tanzania ni kati ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano hayo, hivyo ni jukumu la wachezaji kujituma ili kuhakikisha wanarejea nyumbani na ushindi.

“Nina matumaini makubwa na kikosi hiki, nimeangalia idara zote zimekamilika hasa safu ya ushambuliaji,  nimemuona Kichuya hapa na Ajib, naamini hamtawaangusha Watanzania, pigeni kila mtakayekutana naye,” alisema Mwakyembe.

Alisisitiza kwa kuwataka wachezaji wa kikosi hicho kuzingatia nidhamu na kutomdharau mpinzani wao yeyote watakayekutana naye katika michuano hiyo kama njia sahihi itakayowafanya watimize lengo.

Mwakyembe aliahidi  kwenda Kenya kuishangilia timu hiyo endapo itafanikiwa kushinda mechi mbili mfululizo kwa kuanzia na Libya.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, aliahidi kutoa bonasi kwa timu hiyo kwa kila hatua itakayofuzu, akisema  lengo ni kuwahamasisha wachezaji wajitume zaidi.

Naye kocha mkuu wa timu hiyo, Ammy Conrad ‘Ninje’, alisema maandalizi yao kuelekea michuano hiyo yamekamilika.

“Tupo tayari kwa michuano, tumejipanga kupambana kila mechi na kushinda, hili linawezekana kwa sababu tunachotaka ni kuchukua ubingwa wa mashindano haya,” alisema.

Alisema  amebadilisha mfumo wa kikosi hicho akifichua kuwa atatumia ule wa 4:4:2 ‘Diamond System’ ingawa wanaweza kubadilika kulin

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles