24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel yaja na ‘Airtel Simu Bima’ kuwezesha wateja

jackson-mmbandoNa Mauli Muyenjwa-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya UAP, wamezindua huduma itakayowasaidia wateja wote wanaotumia simu za smartphone kuziwekea bima na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money.

Huduma hiyo mpya nchini itajulikana kama ‘Airtel Simu Bima’ ambayo itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, alisema: “Leo Airtel tumeongeza sababu nyingine kwa wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu, sasa wateja wote wenye simu orijino za smartphone wataweza kusajiliwa na huduma ya ‘Airtel SimuBima’ ambapo mteja mmoja anataweza kusajili hadi simu mbili katika mfumo huu.

“Ikitokea mteja ameibiwa simu yake au kuipoteza, basi kupitia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia mteja huyo pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena,” alisema Mmbando.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa UAP, Raymond Komanga, alisema: “Tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa bima ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na kutujulisha sisi, tutalipa simu za hadi shilingi milioni moja na laki tano,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles