|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kupitia kitengo chake cha rasilimali watu imefanya bonanza la michezo lililowashirikisha wafanyakazi wake kwa lengo la kujenga afya zao na kuongeza ushirikiano eneo la kazi.
Mara baada ya bonanza hilo, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu, Mubarak Kibarabara amesema wamefanya hivyo kwa kuwa Airtel inatambua jitihada za serikali zinazosisitiza kuboresha na kuweka mzingira rafiki sehemu za kazi.
“Pia Airtel tunafahamu sana umuhimu wa michezo na mazoezi kwa afya za wafanyakazi wetu, ndiyo maana tumeona ni vyema kukutana kwa michezo kama hivi ili kuwasaidia wafanyakazi ‘kurelax’ na kubadilishana mawazo wakiwa katika mazingira tofauti,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Aritel, Sunil Colaso amewapongeza washindi wa Bonanza hilo na kuwataka wafanyakazi wake kuzingatia umakini pale wanapohudumia wateja.
“Niliona mwanzo mlianza kushindania kawaida mno lakini baada ya ushindani kupamba moto wote mkawa makini na mkawa mnalenga kweli kweli mpira usiende nje, sasa mnapaswa umakini huo pia muuzingatie kwenye kutoa huduma kwa wateja wetu wote tunapaswa kuwa makini hivi hivi,” amesema Colaso.
Katika Bonaza hilo, wafanyakazi hao walishiriki mchezo wa kupigiana penati kwa wasichana wote kwa mgawanyo wa vitengo vyao vya kazi kikiwemo kitengo cha Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu kinachoundwa na Rasilimali Watu na Udhibiti Huduma, Kitengo cha Masoko, Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Mauzo, Ununuzi na Ugavi na Kitengo Fedha na Mipango.