24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel Divas yatembelea kikundi cha Sauti

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Airtel Divas
Umoja wa kikundi cha wanawake cha Airtel Divas

jana wametembelea kikundi cha Sauti ya Wanawake Walemavu Tanzania (SWAUTA), katika banda lao lililopo katika maonyesho ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

Airtel Divas wamefanya hivyo zikiwa zimepita siku chache tangu walipofanya harambee ya kukiwezesha kikundi hicho kupata fedha za kulipia banda katika viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Sabasaba, ili nao kuonyesha bidhaa zao kwa Watanzania.

Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo, Meneja Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi ambaye pia ni mwanachama wa Airtel Divas, alisema kuwa wanajihisi wenye furaha baada ya kuona wamefanikiwa kuwawezesha wanawake walemavu.

“Tunayo furaha kuona tumeweza kuwasaidia kina mama wenzetu kutimizia lengo lao na kuwapa nafasi ya kuweza kuonyesha ubunifu wao, uwezo wao na kazi zao za mikono kwa washiriki na wateja wa ndani na nje wanaotembelea Maonyesho ya Sabasaba.

“Ni matumaini yetu kuwa fursa hii ya kuonesha na kujitangaza hapa Sabasaba itawawezesha kufikia malengo yao ya kutanua wigo wa biashara zao na kupata masoko na kuuza bidhaa zao kwa wingi zaidi,” alisema Buyumi.

Meneja huyo wa Airtel Divas aliwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi ili kuwaunga mkono kina mama hao katika banda lao lililoko kwenye jengo la Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake, Mwanachama wa Umoja wa Sauti ya Walemavu Tanzania, Adelina Mluge, alisema: “Tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuwepo katika mazingira mazuri ukilinganisha na ilivyokuwa miaka iliyopita. Mpaka sasa tumeweza kupata wateja wengi wakipita hapa kuona na kununua bidhaa zetu kwa wingi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles