29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

AFRIKA KUHAMIA NGUVU ZA NYUKLIA

Na Joseph Lino,

Wakati Afrika na haswa Afrika  Mashariki katika mbio za kuelekea kupata nguvu za nyuklia Tanzania bila sababu ya msingi kuonekana kunyo,g’onyea na kujidhalilisha katika malengo ya kupata nishati hiyo muhimu  kwa maendeleo ya uhakika ya  viwanda.

Nchi za Kenya na Uganda wako mbele kuingia kinyang’anyiro cha kuwa na nguvu za umeme kutokana na nyuklia Tanzania yeneye madsini ya uranium ya uhakika na grafiti pekee ya jumbo inajirudisha nyuma na kufikiria kuwa na kituo cha utafiti  wa urani pekeechenye nguvu ya Megawati 1000 tu.

Kenya na Uganda wako mbele na hivyo wataifanya Tanzania kuwa soko lao la kuuza umeme badala ya kununua kwake kwa vile ina hazina ya urani ya kutosha kwani ni ya saba duniani kwa uwingi na hivyo kusababisha maswali mengi bila majibu kuhusu unyonge wake mbele ya mataifa.

Kazi ya ujenzi ya vituo na uhamishaji wa teknolojia ya nguvu za nyuklia itatolewa na kampuni ya Kirusi ya Rosatoma ambayo ni maarufu duniani kote kwa teknolonjia hiyo.

Kampuni ya nishati ya nyuklia ya Rosatom mwaka jana ilitangaza kufanya makubaliano na nchi mbalimbali zaAfrika mpango wa  kutafiti, kutoa mafunzo,  kujenga na kuzalisha nishati ya nyuklia kutokana  na kugundulika kwa madini ya urani kusini mwa Tanzania katika mto Mkuju Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.

Mikataba imefanywa na nchi za Kenya , Uganda, Tanzania, Ghana, Zambia  Afrika Kusini na Nigeria kujenga vituo vya ukubwa mbalimbali na kwa bei mbalimbali lakini kwa ujumla Tanzania ndio ilikuwa na malengo  duni ya kituo kidogo cha MW 1000 cha utafiti wakati wengine wakijinasibu kwa urefu na mapana kuupata umeme huo wa uhakika. Kwa nini hali hiyo bado ni kitendawili na juhudi zilipofanywa hakauna mtu aliyekubali kusema lolote Wizarani.

Kutokana na taarifa ya Makamu Rais wa Uranium One, Andre Shutov, Kampuni mama ya Rosatom kutoka Urusi  inatarajia kuanzisha mpango wa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme ya nyuklia nchini Uganda ifikapo mwaka 2034 wa MW  4300 kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 26.

Lengo kuu kuzalisha urani

Ripoti ya AF-Consult Switzerland inasema  Uganda itahitaji kuwekeza dola za Marekani bilioni 26 kujenga mtambo wa nyuklia wenye kuzalisha megawati 4,300 kutoka kwenye nishati ya nyuklia ifikapo mwaka 2040.

Kwa upande wa Tanzania, Makamu Rais wa Uranium One ambayo ni kampuni tanzu ya Rosatom,  Andre Shutov, alisema watajenga kituo cha utafiti cha nyuklia awamu ya kwanza kwa ajili ya maendeleo ya nyuklia nchini. Hayo yamekamilishwa na mkataba wa makubaliano uliosainiwa  kimya kimya tarehe  31 Oktoba  mwaka jana kutokana na ripoti ya Gazeti la Sputnik  la Urusi.

“Kuzalisha urani itakuwa lengo letu kubwa, na uzalishaji wa kwanza utafanyika mwaka 2018, matarajio ni kuzalisha mapato ya kampuni na Tanzania. Hatuwezi kufanya kosa, tunapotarajia kufikia uzalishaji katika kipindi cha miaka miwili au mitatu ijao, alisema Shutov.”

Hizi ni habari  njema kwa nchi ambayo  iligomewa na wakubwa kwa kisingizo cha uharibifu wa mazingira wasichimbe urani iliyojaa kwenye mbuga ya Selous Game Reserve (SGR).

Kufikia lengo la kuchimba hazina hiyo ya madini ya Urani Kampuni ya Uranium One ilishapata kibali kutoka serikali cha kutafuta na kuchimba urani iliyopo Mto Mkuju karibu na hifadhi ya Selous katika eneo lililomegwa  kutoka hifadhi hiyo ili litoe mchango katika ukuaji uchumi wa Tanzania.

Tanzania inaangalia uwezekano wa kuwa na mitambo ya kuzalisha umeme wa nyuklia ifikapo 2025 ambayo imekiswa kugharimu dola bilioni 4.

Sio siri gharama za ujenzi wa uzalishaji wa umeme wa nyuklia ni kubwa mno na kutumia teknolojia ghali sana lakini baada ya hapo mambo huwa poa na hakuna gharama zaidi ya mishahara na matengenezo ya kawaida.

Kwa nchi kama Tanzania kiasi cha dola bilioni 4 za mradi wa umeme wa nyuklia ni kidogo  sana ukilinganisha na Uganda, Kenya na Zambia lakini hao wengine wanapata umeme mwingi zaidi nakuigeuzia kibao Tanzania kuwa soko la umeme wao wa ziada.

Umuhimu wa mitambo ya nyuklia huwa na gharama ndogo ya uendeshaji  mradi  utakapokamilika.

Kwa upande wa Kenya, Nuclear Electricity Board, inasema kuwa nchi hiyo itahitaji kiasi cha dola bilioni 20 kujenga mitambo ya nyuklia ifikapo 2023 yenye megawati 4,000. Rosatom tayari imesaini mkataba na Kenya katika kushughulikia mradi wa umeme wa nyuklia ikiwemo kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa gharama ya dola bilioni 20.

Changamoto za mazingira

Hata hivyo, wanaharakati wa masuala ya mazingira kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki wanahofu ya kuhusiana na taka za mionzi ya nyuklia (radiation waste) na  wanapinga ujenzi na kuonya  kuwa taka  za hatari zinaweza kupasua miamba na mwishowe kuwafikia wananchi kwani hakuna cha kuweza kuzuia upenyaji huo.

Hivi basi wanadai kwa  kishindo kuwa mgodi wa Urani kusini mwa Tanzania, unahatarisha kundi  la wa wanyama pori na wananchi wanaoishi kuzunguka hifadhi ya Seolus ambayo ni kubwa kuliko zote barani Afrika

Taasisi ya World Wildlife Fund (WWF) tayari imeelezea hofu ya uchimbaji wa urani  na kusema kuwa shughuli za uchimbaji  huo ambazo zinaendelea Mkuju zinaweza kuleta athari za uchumi na afya za muda mrefu kwa watu wanaoishi maeneo hayo na Tanzania kwa ujumla.

MTANZANIA kupitia Gabriel  Mushi hapo awali ilifanya mahojiano na Mantra Resources Ltd ambao walikuwa wanamiliki shughuli ya Mradi wa Mkuju kabla ya kuuza kwa Uranium One  na walijibu kuwa hakuna shida kwenye mazingira kwani watatumia teknolojia ya hali ya juu isiyostahili kutiliwa shaka.

MANTRA: Tutatumia teknolojia ya kisasa kuchimba Uranium na kutoa takwimu za mradi kama ifuatavyo.

“Mwaka 2013 serikali ilithibitisha kuwapo kwa hifadhi ya tani milioni 175.8 za mashapo ya madini hayo. Kiasi hicho ni sawa na kilo milioni 52.5 za uranium kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya nishati na madini ni kwamba mashapo hayo yanawezesha uhai wa mgodi kwa zaidi miaka 12.

Hata hivyo athari katika uchimbaji wa madini hayo, uhifadhi na hata usafirishaji wake ni mojawapo ya changamoto ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na baadhi ya wanaharakati nchini kwa madai kuwa yataharibu uhai wa viumbe hai wakiwamo binadamu.”

MTANZANIA lilizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Frederick Kibodya wakati huo ili kupata ufafanuzi namna gani imejipanga kulinda afya za Watanzania na wafanyakazi wake kwa ujumla.

MTANZANIA: Mradi umefikia katika hatua gani sasa?

KIBODYA: Mradi unaendelea kufanyiwa utafiti katika nyanja ya kutumia teknolojia ya kisasa ambayo itaepusha uchafuzi wa mazingira na usalama wa hali ya juu na uendelezaji wa kimazingira, hapa nchini mradi huu umefanyiwa utafiti miaka saba iliyopita na umeanza kubuniwa uendelezaji wake, kwa kushirikiana na kampuni ya Rosatom ambayo itaweza kutekeleza mradi wetu kwa usalama na kuzingatia masharti yote ambayo yanatakikana.

Tumewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 200 (zaidi ya Sh bilioni 436), ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezeka kama inavyotakikana.

MTANZANIA: Ni teknolojia gani hiyo ya kisasa na itakuwa inatumika vipi?

KIBODYA: Tunatarajia kuchimba madini ya uranium kwa kutumia teknolojia ya kisasa iitwayo ‘In-Situ Recovery (ISR)’ ili kuzuia madini hayo yasiharibu mazingira na uhai wa viumbe wengine. Ni teknolojia ambayo haitaacha madhara yoyote katika ardhi ya Tanzania.

Ni kwamba teknolojia hii ya ISR ambayo itatumika katika uchimbaji wa madini ya uranium haitahusisha ubomoaji au uchimbaji wa jumla wa udongo. Kwamba unatoboa shimo kama nusu futi unaingiza kimiminika ambacho kinaenda kuyeyusha yale madini alafu unafyonza yale madini, ukiacha ardhi yako ikiwa katika hali ileile bila kuharibika.

Kwa hiyo ni teknolojia ya kisasa inatumika katika uchimbaji wa madini ya aina mbalimbali zaidi katika urani kwani inadhibiti madini yote ikiwamo uwezekano wa yale mabaki ya madini. Hivyo hakutakuwa na mabaki, kwani itakuwa imeshapatikana, kwa hiyo tunafanyia utafiti ambao  umekaribia kukamilika na tunatarajia kuitumia katika uchimbaji wa urani ya Mkuju.

MTANZANIA: Kwa maana hiyo mradi huu unatarajiwa kukamilika lini na kuanza shughuli za uchimbaji?

KIBODYA: Mradi huu sasa upo katika hatua za mwisho za majaribio hivyo na katika kipindi cha miaka miwili ijayo madini hayo yataanza kuchimbwa kwa majaribio na baadae utaanza uchimbaji wa kibiashara.

MTANZANIA; Serikali itafaidika vipi na uwapo wa mgodi huu?

KIBODYA: Ni dhahiri kuwa kuna faida kubwa katika mradi huu hasa kiuchumi kwani utaleta mapato kwenye nchi, na washiriki mbalimbali, tutauza nje madini haya, uwekezaji utakuwa mkubwa zaidi ya dola za Marekani bilioni moja, watanzania walio wengi watapata ajira katika huo mradi, pia kutakuwa na teknolojia mpya ya kisasa ambayo watuwataitumia na kujifunza katika madini hayo ya urani.

Lakini pia mbali na serikali kufaidika kuna suala la ajira, kwani baada ya mradi huu kukamilika tutaweza kuajiri zaidi ya watu 1,000. Sasa kuna wafanyakazi zaidi ya 100 ila bado wapo wakandarasi wanaokuja na kuondoka katika kutekeleza shughuli mbalimbali za mradi.

MTANZANIA: Inasemekana madini haya yanatumika pia kuzalisha umeme, je, Unafikiri Tanzania itaweza kufikia hatua hiyo na kutatua tatizo la umeme nchini?

KIBODYA: Ni kweli kuwa tutaweza kufikia hatua hiyo iwapo serikali ikiamua. Ni kwamba mradi huu umetengenezwa kwa uzalishaji wa kitu kinachoitwa yellow keki, (uranium oxide), ni kitu kinapatikana kwenye ardhi kama kilivyo, ili ufikie hatua ya kuzalisha umeme kuna mchakato mkubwa mambo mengi, tutahitaji vitu kama mashine,  mitambo,  rasilimali watu  ya hali ya juu na mengine.

Tanzania ina nafasi nzuri ila inatakiwa kujipanga na kuweka mambo yote sawa. Tunatambua kuna tatizo la umeme ila umeme unaotokana na urani ni mzuri hauharibu mazingira, hivyo ili kuhakikisha ‘Tanzania ya viwanda’ lazima kuwepo na umeme wa uhakika kutokana na madini hayo, hivyo lazima kuweka maandalizi yote kutumia rasilimali hii.

 Lakini pia madini hayo yanatumika katika matumizi ya kiutafiti na kitabibu kwa wagonjwa wa kansa ambao hutibiwa kwa kutumia mionzi.

MTANZANIA: Mantra Tanzania inauzoefu gani katika uchimbaji wa madini hayo?

KIBODYA: Ni kwamba Mantra Tanzania ni kampuni ambayo ipo chini ya usimamizi wa makampuni mawili makubwa duniani yanayojishughulisha na uchimbaji wa madini hayo zaidi ya miaka 70.

Kwanza ni kampuni ya Rosato m inayomilikiwa na Serikali ya Urusi ambayo inashughulikia masuala ya nguvu za nyuklia. Rosato pia inamiliki kampuni inayoitwa Uranium One ambayo inashughulikia masuala ya miradi yote ya urani nje ya Urusi. Mojawapo ya miradi hiyo ni Mkuju River Project uliopo Tanzania, Uranium One inamiliki migodi katika nchi za Kazakstani na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles