26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

AFIC yaiomba Serikali kutunga sera zinazolinda wanahabari Wanawake

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Africa Freedom of Information Centre(AFIC), imeiomba Serikali kutunga na kutekeleza Sheria na Sera zinazozingatia jinsia ili kuboresha usalama wa wanahabari mahala pa kazi hasa kwa wanawake.

Hayo yamebainishwa Juni 15, jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Ufuatiliaji na Tathimini wa (AFIC), Charity Komujjurizi, ambapo amesema kuwa wamebaini waandishi wa habari wanawake ni wachache ukilinganisha na wanaume kwenye tasnia hiyo.

“Mwitikio wa kijinsia unapaswa kuoneshwa katika taasisi za Serikali zinazohimiza uhuru na usalama wa vyombo vya habari katika kila nchi,” amasema Charity.

Amesema kutokuwepo kwa sheria, sera na mifumo mahususi ya kitaasisi inayoshughulikia usalama wa wanahabari wanawake unarudisha nyuma mapambano ya vitisho na vitendo vya ukatili dhidi ya waandishi wa habari wanawake.

Charity amesema Waandishi wa Habari wanawake wanafanya kazi sawa na wana uwezo sawa na wanaume lakini wanalipwa kidogo na hawapati ajira za moja kwa moja.

Aidha, amesema waandishi wa habari wanawake wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ikiwemo ukatili wa kijinsia, ukatili wa kingono pamoja na ukatili wa kimtandao.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari, Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa- Tan), Salome Kitomary alisema bado kuna changamoto ya idadi ya waandishi wa Habari Wanawake na katika ngazi za maamuzi ni ndogo katika ngazi za juu ukilinganisha na wanaume.

Amesema usalama wa waandishi wa Habari kwenye suala la kipato bado ni changamoto (Sera, sheria na taratibu) hivyo ni muhimu kufanyike maboresho ya sera ndani ya vyombo hivyo ili ziwe jumuishi kwa wote.

“Ni lazima sisi waandishi wa habari tuchukue hatua, vyombo vyetu vya habari vifanye jitihada za kuboresha mazingira ya kufanyia kazi, kuwawezesha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao ya kila siku,” amasema Kitomari.

Amesema sheria ni sehemu ndogo ya matatizo yanayowakabili waandishi wa habari hivyo ni muhimu mabadiliko yaanze kwa kila mmoja wao na mifumo ya wanawake na wanaume wanapokutana na changamoto sehemu za kazi inapaswa ziweke wazi kwenye vyombo vya habari.

Naye Meneja wa Mipango na Mikakati wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA), Slyvia Daulinge alisema bado kuna kazi ya kuhakikisha usalama kwa waandishi wa Habari hasa wanawake unafanyika katika masuala ya jinsia na watahakikisha wanajengea uwezo wanahabariwa wanawake kupigania masilahi yao na kupinga manyanyaso.

“Sasa hivi masuala ya ukatili si tu ukatili wa kinafsi, kihisia lakini kuna masuala ya kipato duni na ukatili wa kutokupewa nafasi, kutopata stahiki zao ukilinganisha na kazi wanazofanya,” amesema Katomary.

Upande wake Mkurugenzi Uchechemuzi(TWAWEZA), Risha Chande amasema jamii inapaswa kulea watoto wao kwa kujiamini ili kuweza kuzungumzia changamoto anazoweza kuzipata katika mazingirayoyote.

Alisema kupitia utafiti wamebaini kuwa unyanyasaji mtandaoni unaongezeka na kurudisha nyuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles