23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Adama Dieng atoa tamko dhidi ya ISIL

genocide-adama-dieng

Mshauri Malum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia Mauaji ya Halaiki, Adama Dieng, amekemea vikali hali ya dharau iliyokithiri dhidi ya haki za binadamu zilizokubalika kimataifa na hali ya kudharau sheria za kimataifa za kutoa huduma unaofanywa na Taifa la Kiisalamu la Iraq na Levant(Islamic State of Iraq and the Levant(ISIL), kupitia hatua zilizochukuliwa na ISIL hivi karibuni katika muktadha wa vita vinavyoendelea ndani na kuzunguka Mosul.

Taarifa za hivi karibuni zimedai ISIL imeshiriki katika; utoroshwaji na mauaji ya makundi makubwa ya raia, kuwatumia raia kama kinga wakati wa vita na viongozi wa ISIL kuhamasisha ukatili katika jamii zao.

Kumekuwa na ripoti kuhusu matumizi ya silaha za kemikali na adhabu za pamoja kutolewa kwa walinzi wa usalama wa Iraq pamoja na ndugu zao.

Tarehe 31 Oktoba, ripoti zilizopatikana nchini humo ziliandika kwamba ISIL ilijaribu kuhamisha watu wengi wapatao 25,000 kutoka mji wa Hamam al-Alilhadi wilaya ya Talafar, wilaya ya Mosul na katika mji wa Abusaif ambapo ISIL imeweka makao ya kikosi chake cha vita na ambapo mauaji ya halaiki ya raia yanafanyika.

Mshauri huyo amesema kwamba tuhuma zilizopo sasa zinatosha kwa hatua kuchukuliwa mara moja.

Amerejea tena ombi lake la ushahidi kwa makosa ya kijinai kuwekewa kumbukumbu sahihi na kutunzwa kwa ajili ya uwezekano wa kutumika na mahakama ya haki(Court of Justice) katika siku zijazo.

Vilevile, ameikumbusha Serikali ya Iraq kwamba operesheni za vita lazima ziendeshwe kwa kuheshimu vilivyo sheria ya kimataifa pia ameelezea dukuduku lake kuhusu uwezekano wa kushambuliwa kwa jamii ya Wa Sunni kufuatia ongezeko la hatari la vikundi vya waasi wanaotumia silaha ambao wanadai kulinda makundi ya kikabila na ya kidini katika jamii.

“Iraq inakabiliana na changamoto, iwapo zitashughulikiwa, itakuwa ni fursa nzuri ya kupanda mbegu za Amani kwa ajili ya Amani ya baadae,” alisisitiza Dieng

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles