26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

ACT- Wazalendo waja na siasa mpya

Zitto-KabweNa Mwandishi Wetu, Iringa
CHAMA cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Wazalendo), kimeibuka na mikakati mipya ikiwemo kuhamasisha kuanzisha kampeni maalumu ya kuwataka Watanzania kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga kura kupitia mfumo wa elekroniki (BVR), kwa matangazo ya redio.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ikabadili hali ya kisiasa ambapo vyama vingine vimekuwa vikitumia zaidi mikutano ya hadhara lakini chama hicho sasa kimebuni njia mpya ya kutangaza kupitia njia hiyo.
Wakizungumza jana mjini hapa, baadhi ya wananchi wa mikoa ya Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara ambo hivi sasa walisema kuwa tangazo hilo limewafanya wapate hamasa ya kujiandikisha katika daftari la BVR.
“Tumefurahishwa na kitendo cha ACT-Wazalendo, kutuhamasisha bila kutumia matusi, kejeli wala vurugu bali ujumbe mzuri,” alisema Daud Kiswaga mkazi wa Iringa.
Alisema aliposikia tangazo hilo alihamasika kwa ajili ya kujiandikisha yeye na familia yake pasi na shaka na hata kuhisi wajibu wake kama raia mwema kwa nchi yake.
“Tangazo linalochezwa katika radio mbalimbali wanasikika watu wakisikitishwa na namna idadi ya Watanzania inavyopungua kila mwaka wa uchaguzi kulinganisha waliojiandikisha na wanaojitokeza kupiga kura,” alisema.
Katika tangazo hilo, inaelezwa kwamba mwaka 2000 Watanzania milioni 10 walijiandikisha kupiga kura lakini ni watu milioni 8 tu ndio waliopiga kura, huku mwaka 2005 Watanzania milioni 16 walijiandikisha kupiga kura lakini ni watu milioni 11 tu ndio waliojitokeza kupiga kura.
Na kwa mwaka 2010 Watanzania milioni 20 walijiandikisha kupiga kura lakini ni Watanzania milioni nane tu ndio waliopiga kura.
Katika kuweka sawa tangazo hilo inaelezwa kwamba isingekuwa rahisi kwa watu wengi kupiga kura kwa sababu walishakatishwa tamaa na vyama vilivyokuwepo.
“ACT ni chama kipya chenye harakati mpya za kuwaunganisha Watanzania kusimamia rasilimali zao. Ndio maana tumekuwa tukiwataka Watanzania wote wazalendo kujiandikisha na wawe tayari kwenda kukupigia kura wakati utakapofika,” alisema mmoja wa viongozi wa ACT
Hivi karibuni chama cha ACT-Wazalendo, kilifanya uchaguzi wake mkuu mwishoni mwa Machi mwaka huu, ambapo waliwachagua viongozi wake akiwemo kiongozi wa chama Zitto Kabwe, Mwenyekiti Anna Mghwira, na Katibu Mkuu Samson Mwigamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles