24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

“Acheni kuchafua meza kwenye futari na daku” Sheikh Mustwafa

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waislamu nchini wametakiwa kufuata maelekezo ya mtume Muhammad (SAW) wakati wa Futari na Daku, badala ya mazoea mabaya ya kula na kujaza tumbo kwa sampuli mbalimbali za vyakula.

Ukumbusho huo muhimu umetolewa leo na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Faraji Mustwafa kwenye hotuba ya Ijumaa Masjid Gaddadi jijini Dodoma ambapo pia Sheikh ameeleza kwa kina faida ya kufufuru kwa tende na maji kama mtume alivyoelekeza.

Kwenye hotuba hiyo Sheikh Mustwafa amekemea vikali tabia na mazoea ya kupika vyakula vingi na kueleza kwamba haina uhusiano na swaumu kwa namna yoyote akalaani desturi mbaya ya kuwatumikisha wanawake kutwa nzima kuandaa sampuli tele za vyakula huku majirani na yatima wakiachwa pasina msaada wowote.

“Akinamama wanaandaa Maandazi, kababu, chapati, viazi, keki, ndizi, uji, chai, juisi, mihogo tambi… Hawana muda hata wa kwenda msikitini. Waislamu acheni israafu. Mnadhuru miili yenu kwa kula ovyo na mnapoteza maana ya swaumu” amesema.

Sheikh Mustwafa amewaambia waislamu waliofurika msikitini hapo kwamba swaumu, futari na daku ni ibada na kila ibada lazima ifanyike kama dini inavyotaka na si vinginevyo.

Amesema tende ni tunda lenye faida kubwa kiafya. Ina virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na madini na vitamini ambavyo ni muhimu sana kwa afya ya mwanadamu.

Amesema badala ya kujifaharisha kwa kula sana watoe sadaka kwa wasio na uwezo.

“Acheni kuchafua meza, tumbo ligawiwe kwa ajili ya chakula, maji na hewa. badala yake saidieni maskini, yatima, wajane na wasiojiweza,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles