24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

ACACIA YAKAMILISHA UJENZI WA MAKTABA NYANG’WALE

Na HARRIETH MANDARI

MGODI wa Dhahabu wa Bulyankulu Wilaya ya Kahama, umekamilisha ujenzi wa maktaba   ya jamii katika Shule ya Msingi ya Bupamba na kuikabidhi iweze kutumika.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu wa Kampuni ya Madini ya Acacia, Benedict Masunzu, alisema wananchi wanapaswa kuitumia mkataba hiyo   kujenga utamaduni wa kujisomea kwa kuwa kufanya hivyo kunaongeza maarifa.

Alisema maktaba hiyo ambayo itatumika na watu wote, ina vitabu mbalimbali vikiwamo vya mbinu za kilimo bora cha kisasa, ufugaji na ujasiriamali.

Iwapo itatumika vema inaweza kuwasaidia kujenga maarifa, alisema.

Alisema maktaba hiyo imejengwa katika jengo ambalo awali lilkuwa la walimu wa Shule ya Msingi Bupamba na limegharimu   Sh milioni 23.

Masunzu alisema  ukarabati huo   na ununuzi wa vitabu na samani umefanywa na mgodi huo kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Serikali la Read International.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’wale, Fabian Sospeter, akizindua mradi huo, aliwataka wanafunzi na wananchi wa wilaya hiyo kuitumia maktaba hiyo vizuri   kuleta maendelelo kwa vile kusoma ni maarifa.

“Vipo vitabu mbalimbali humu, vya  taaluma, kilimo na vingine vingi ambavyo wakulima na wajasiriamamli mnapaswa kutenga muda mfike maktaba kujisomea na kupata ujuzi wa mbinu za kisasa za uendeshaji shughuli,”alisema.

Pia aliwasisitiza  wazazi na walezi kujisomea vitabu vya lishe bora kwa watoto kuondokana na tatizo la ukosefu wa lishe bora kwenye jamii hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Read International, Magdalena George, alisema  shirika hilo limesaidia ujenzi wa maktaba zipatazo 95 kwenye shule za msingi na sekondari 1,000 nchini.

Alisema shirika bado lina mpango wa kuanza kutoa elimu kwa walimu  ya jinsi ya kutunza maktaba hizo na  kuhamasisha wananchi   kupenda kujisomea vitabu.

“Ni matuamaini yangu kuwa kupitia walimu hao wataweza kuwashawishi wasomaji angalau 700 kuingia na kujisomea vitabu na majarida mbalimbali.

“Hata ikiwezekana itakapokamilika   wasomaji 8,000 wawe wameingia kwenye maktaba hii,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles