26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

MGOMBEA CHADEMA KUPINGA MATOKEO MAHAKAMANI

Na HARRIETH MANDARI-GEITA

MGOMBEA wa Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Demoktrasia na Maendelea (Chadema), Bwire Vitara amepinga matokeo ya uchaguzi wa udiwani katika Kata ya Senga wilayani Geita   na kudai akakwenda mahakamani.

Akizungumza   baada ya matokeo kutangazwa na Mgombea wa CCM kuongoza, alisema   Chadema hakikubaliana na matokeo hayo hivyo aliamua kutosaini fomu za matokeo.

Alisisitiza watakwenda kuitafuta haki yao kwa kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo hayo.

“Kulikuwa na manyanyaso kutoka kwa wasimamizi uchaguzi, pia baadhi ya mawakala kutoka vyama vya upinzani kwa baadhi ya vituo walizuiliwa kwa   saa saba  kwa madai kuwa hawakuwa halali katika kituo cha Senga jambo ambalo tumelipinga vikali na tutachukua hatua za  sheria,”alisema.

Akijibu tuhuma hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ally Kidwaka, alisema uchaguzi umekwisha salama,

Kidwaka alisema kulitokea matatizo miongoni mwa baadhi ya mawakala ambao walikiuka taratibu za usimamizi wa uchaguzi hivyo kushindwa kufika mapema katika vituo vyao vya kazi.

“Kanuni ya sheria za uchaguzi namba 42 ya mwaka 2015, inavitaka vyama vya siasa kupanga mawakala wake  na kuhakikisha wamefika eneo la kazi mapema.

“Kwa hapa vyama hivyo viliwapanga vituo vya mbali hivyo kuwa sababishia kuchelewa kufika vituo,” alifafanua.

Katibu wa CCM mkoa wa Geita alikanusha madai ya vyama vya upinzani kuwa   CCM kilishinda kwa rushwa akisema tuhuma hizo zinatokana na hofu ya kushindwa tu.

Mgombea wa CCM, Tumbo Edward aliahidi kuyafanyia kazi matatizo yote ya  maendeleo yanayoikabili kata hiyo.

Kata hiyo imekuwa  haina diwani kwa muda mrefu kutokana na aliyekuwepo awali, Joel Ntinginya ambaye alitolewa baada ya kukiuka kanuni na sheria za uchaguzi kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles