27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Washindi 40 wa droo ya pili NMB MastaBata watangazwa

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB, imetangaza washindi 40 wa Sh. 100,000 kila mmoja wa droo ya pili ya Kampeni ya NMB MastaBata 2020, inayochagiza matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR miongoni mwa wateja wa benki hiyo.

NMB MastaBaata, ni kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24 mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo za pesa, simu janja ‘smartphone’, jokofu, runinga pamoja na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

Droo ya pili ya kampeni, imefanyika Makao Makuu ya NMB, jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Rasuli Masudi, aliyewahakkishia washiriki na washindi mchakato unaozingatia sheria zote kuwapata.

Meneja  Mwandamizi Idara ya biashara za kadi wa Benki ya NMB, Manfred Kayala (katikati) akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya pili ya Promosheni ya Mastabata iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha uzalishaji Kadi wa Benki ya NMB, Sophia Mwamwitu na kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Rasuli Masudi.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara za Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema katika kipindi chote cha kampeni hiyo, watakabidhi zawadi kwa jumla ya washindi 40 watakaojishindia fedha taslimu 100,000 kila wiki.

Pia, alifafanua kuwa NMB MastaBata itawazawadia washindi 15 simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Shilingi 2,480,000 kila mwezi, pamoja na zawadi kuu itakayotolewa katika fainali ya kuhitimisha kampeni hiyo.

“Zawadi kubwa kwenye kampeni hii ni ile ya washindi 15 pamoja na wenza wao kushinda safari ya utalii wa ndani iliyolipiwa kila kitu na NMB, ambapo mshindi na mwenza wake watapata nafasi ya kutembelea Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

“Aidha, washindi wa fainali tutawapa ruksa ya kuchagua utalii wa ndani au kuchukua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu la Milango Miwili, Kompyuta Mpakato, Simu Janja (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave,” alisema Kayal.


Kwa upande wake, Masudi kutoka GBT, aliwatoa shaka wateja wa NMB wanaoshiriki NMB MastaBata, akisema mchakato wa kutafuta na kutangaza washindi, unafanyika kisheria chini ya bodi hiyo na kwamba hakuna ubabaishaji katika hilo.

Aliwataka wateja wenye NMB Mastercard na Masterpass QR, pamoja na wote wanaofanya maaaanunuzi mbalimbali kupitia POS, kushiriki kinyang’anyiro hicho mara nyingi wawezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi za wiki, mwezi na hata ‘grand finale’ Februari 2021
Katika droo hiyo ya Ijumaa Desemba 11, washindi 40 waliotangazwa na kupigiwa simu nii pamoja na Samwel Kilua, Mgonja Tumaini, Msindai Wazael, Saria Fulgence, Joachim Mabula na Alex Katan

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles