ABUJA, NIGERIA
Taarifa kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa maofisa wa Serikali wanaokabiliwa na shutma za ufisadi wamekuwa wakibadilika ghafla na kuwa walemavu huku wengine wafariki pindi wanapofika mahakani.
Inaelezwa kuwa wanasiasa au maafisa wa ngazi ya juu wamekuwa wakitoweka kutoka ndani ya mahakama, na wengine wamekuwa wakifika mahakamani wakiwa katika viti vya walemavu au vya wagonjwa – wheelchairs kuomba msamaha au kutaka maelewano.
Wengi wanashutumiwa kwa ubadhilifu wa mali ya umma au ufisadi, kwa mujibu wa BBC maafisa sita wa ngazi ya juu wa serikali ya Nigeria ambao wamegeuka na kuwa walemavu, kuanguka mahakamani huku baadhi wakifariki dunia ikiwamo kuugua wanapohojiwa kuhusiana na tuhuma dhidi yao.
Mwenyekiti wa zamani wa hazina ya taifa ya akiba ya uzeeni nchini Nigeria, Abdulrasheed Maina, ambaye kesi yake imekuwa ikiendelea tangu mwaka 2019, amefariki ndani ya mahakama mjini Abuja baada ya kufika mbele ya mahakama hiyo jana Alhamisi.
Maina alihukumiwa kifungo cha maisha jela na jaji wa mahakama ya wilaya kwa madai ya ubadhilifu wa mali ya umma wa kiasi cha dola bilioni 2.
Video inayosambazwa katika mitandao ya, Maina akitafuna ulimi wake huku akipata tena fahamu baada ya kuanguka na kuzirai.
Maina alikamatwa hivi karibuni katika Jamuhuri ya Niger ambako alirejeshwa nchini Nigeria na polisi ya kimataifa kuendelea na kesi yake baada ya kutoraka alipopewa dhamana.