28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yataka tafiti dawa asilia

Na Aveline Kitomary

Serikali imewataka watafiti mbalimbali kufanya tafiti za dawa asilia ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamesemea leo Novemba 9, 2020 na Mganga mkuu wa serikali, Prof Abel Makubi wakati akimwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Tunahitaji tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali za afya, wakati wa mlipuko wa Covid-19 wengi tulirudi kwenye dawa zetu za asili muda umefika sasa tupate majibu ya kisayansi yatakayotuonesha kwenye zile dawa kulikuwa na kemikali gani.

“Aidha tunatambua kuna dawa nyingi sana za asili zinatumika kutibu pumu, shinikizo la  juu la damu, saratani na mengineyo hivyo tunawakumbusha watafiti na taasisi zetu zote za utafiti kufanya tafiti za dawa hizi ili wananchi wetu wapatiwe taarifa sahihi za dawa hizi,”ameeleza Prof Makubi.

Amesema mchango wa tafiti mbalimbali ni muhimu iwapo utazingatia zaidi ubunifu, ugunduzi wa dawa na chanjo mbalimbali zitakazosaidia kupunguza magonjwa na vifo vinavyozuilika.

Magonjwa yasiyoambukiza(Non-Communicable Diseases) yanaendelea kuongezeka nchini ambapo jumla ya vifo 134,600 viliripotiwa mwaka 2017 sawa na asilimia 33 ya vifo vyote.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41 ambayo ni sawa na asilimia 71 vya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016.

Vifo vinavyotokea nchini vinatokana zaidi na magonjwa ya moyo na shikizo la Damu kwa asilimia 13, kisukari asilimia mbili, saratani asilimia saba na ajali asilimia 11 hali hii kwa ujumla haikubaliki na inatufanya tujumuike katika kujitathimini na kupanga mikakati ya pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles