31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awashukuru Watanzania

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk.John Magufuli amewaomba viongozi wa dini na Watanzania kuendelea kuliomba taifa ili awe kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Taarifa ilityotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais Dk. Magufuli aliwashukuru waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu-Chamwino mkoani Dodoma kwa kuanzisha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Chamwino ambao

umekamilika na kuanza kutumika. Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Janeth Magufuli alitoa shukrani hizo wakati wa misa takatifu ya Jumapili ya 32 ya Mwaka“A”iliyoongozwa na Paroko wa

Parokia hiyo, Padre Paul Mapalala. Aliwashukuru waumini wa madhehebu mengine ya dini waliojitokeza kuchangia ujenzi wa msikiti huo pamoja na Kanisa la Bikira Maria Imakulata Ikulu- Chamwino ambalo ujenzi wake ulifanyika kabla, na amebainisha kitendo hicho kinadhihirisha umoja, upendo na mshikamano wa dhati

walionao Watanzania.
Magufuli alisali ibada ya kwanza

ya Jumapili tangu aapishwe kwa kipindi cha pili, aliwashukuru waumini wa madhehebu yote ya dini kwa sala na dua zao za kuombea mchakato wa uchaguzi mkuu tangu wakati wa kampeni hadi kuapishwa kwake na alisisitiza kuchaguliwa kwake kuwa Rais ni ushindi wa Watanzania wote.

Aliwaomba viongozi wa dini na Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa, na kuiombea Serikali anayoiongoza ili itekeleze ahadi zilizomo katika ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/25 zilizolenga kujenga uchumi imara na ustawi wa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles