29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Ujenzi Stendi mpya Mbezi wafikia asilimia 90

Na Brighiter Masaki

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema Ujenzi wa Stand mpya ya Mabasi ya mikoani ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam umefikia 90% na itaanza majaribio ya kwanza November 25 na kuanza kutumika rasmi November 30, mwaka huu.

Akizungumza na jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kunenge amesema kuwa ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye stand.

“Wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kwenye standi hiyo ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hoteli.

“Zoezi la kutuma maombi ya kufanyabiashara katika standi hiyo limeanza leo November 9 na linatarajiwa kufungwa Novemba 25, mwaka huu,” amesema Kunenge.

Aidha, Kunenge amesema uwepo wa stand hiyo itaendelea kufungua fursa za maendeleo kwa wakazi wa Ubungo hivyo amewataka kujiandaa kwa hilo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles