26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA YAIFUATA PRISONS NA MBINU MBADALA

Na WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Simba kimeondoka jana kwenda mjini Sumbawanga, kuifuata Tanzania Prisons, huku Kocha Mkuu wa Wanamsimbazi hao, Sven Vandenbroeck, akisema amejipanga kukabiliana na kila changamoto ili kurejea na ushindi.

Wekundu wa Msimbazi hao, wameondoka na kikosi cha nyota 22, wakitarajia kukutana
na Prisons keshokutwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mandela, mjini humo.

Wachezaji waliokosekana katika safari hiyo, ni nahodha John Bocco, Gerson Fraga wanaouguza majeraha, Clatous Chama na Pascal Wawa walisafiri.

Simba imekwenda Sumbawanga ikiwa imejirisha katika maandalizi baada ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege na kushinda mabao 3-1 wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumzia mchezo huo, Sven alisema anafahamu aina ya mchezo anaokwenda kukutana nao ni mgumu kutokana na soka wanalocheza Prisons.

Sven alisema Prisons ni timu ngumu na inacheza soka la kutumia nguvu, hivyo kumfanya akiandae kikosi chake kwa mbinu nyingi na kuwaweka wachezaji tifi zaidi.“Prisons nawajua wanacheza soka la nguvu, lakini matumaini ya sisi kufanya vizuri ni makubwa kutokana na kikosi cha wachezaji 22 nilichoondoka nacho.

“Tutahakikisha tunafanikiwa malengo yetu ya kuondoka na alama tatu muhimu, nafahamu ugumu wa mchezo huu utakuwa sawa na mechi nyingine za ugenini tulizocheza,” alisema Sven.

Kocha huyo alisema muda waliotumia kufanya maandalizi ya mchezo huo ni mrefu kuliko mechi nyingine zilizopita, hali inayowapa wachezaji wake kujiamini.

Simba iliyopo nafasi ya pili na pointi 13 katika msimamo wa ligi hiyo, inataka kuendeleza ushindi ili kuifukuzia Azam inayoongoza na pointi 18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles