28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Afya aambukizwa corona

JOBURG, AFRIKA KUSINI

WAZIRI wa Afya wa Afrika Kusini. Dk Zweli Mkhize ametoa taarifa akithibitisha kuwa, yeye na mke wake wameambukizwa virusi vya Covid-19.

Mkhize alisema jana kuwa hivi sasa yeye na mke wake wamejiweka karantini nyumbani, lakini hakubainisha namna alivyoambukizwa virusi hivyo.

Waziri Mkhize aliwataka watu waliokutana naye katika siku kadhaa zilizopita kujiweka karantini, vilevile aliwahimiza wananchi wa Afrika Kusini waendelee kufuata kanuni za kukabiliana na Covid-19, kama vile kuvaa barakoa kwenye maeneo ya umma, na kudumisha umbali wanapokutana pamoja na kunawa mikono mara kwa mara.

Aidha alitoa wito kwa watu wa Afrika Kusini kuendelea kuchukua tahadhari kwani wimbi la pili la corona ni hatari. 

Siku ya Jumapili, Wizara ya Afya ya Afrika Kusini ilitangaza kuwa hadi sasa watu 703 793 wameambukizwa corona nchini humo na waliopona ni  634, 543 au asilimia 90 ya wote walioambukizwa. Waliopoteza maisha kutokana na corona nchini humo hadi sasa ni 18,400.

Wakati huo huo,  kituo cha kudhibiti maradhi cha Ulaya kimesema hadi sasa zaidi ya watu 200,000 wamefariki ndani ya Umoja wa Ulaya na nchi washirika kutokana na virusi vya corona. 

Takwimu hizo za hivi karibuni kutoka kwenye kituo hicho zimeonyesha kuwa karibu watu milioni 4.8 wameambukizwa na jumla ya watu 200,587 wamefariki dunia. Vifo vingi zaidi vimetokea Uingereza, Italia, Uhispania na Ufaransa. 

KENYA YAONYA

Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya Kenya, Mutahi Kagwe ameonya kuhusu hatari ya kuongezeka maambukizi ya covid-19

Kagwe alionya kuwa kuna uwezekano nchi hiyo ikakumbwa na maafa kutokana na wananchi, hasa vijana, kupuuza kanuni za kiafya za kuzuia maambukizi ya corona au Covid-19.

Akizungumza Jumapili, Kagwe alitangaza kesi 685 mpya za corona na aliwaonya vijana waache kucheza na ugonjwa hatari wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Aidha, aliwakosoa wanasiasa ambao wanahutubia mikutano ya hadhara ambayo washiriki hawazingatii kanuni za kimsingi za afya za kuzuia corona kama vile kuvaa barakoa na kutokaribiana. 

Kagwe alibainisha wasi wasi wake kuwa, wananchi, wakiwemo wahudumu wa afya wameanza kurejea katika maisha yao ya kawaida katika hali ambayo janga la corona bado lingalipo.

Alisema kiwango cha maambukizi kimeongezeka kwa asilimi 12 kutoka asilimia 4 wakati serikali ilipopunguza zuio la corona.

Kagwe alisema hadi sasa walipoteza maisha nchini Kenya kutokana na corona ni 832 huku walioambukizwa wakiwa ni zaidi ya 44,000.

Kwingineko, wakazi wa mji mkuu wa Ufaransa, Paris na miji mingine minane wamewekewa marufuku ya kutoka nje kuanzia usiku wa Jumamosi kama hatua ya kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya nchi hiyo kurekodi idadi ya juu ya maambukizi mapya ya watu 32,000 kwa siku moja. 

Kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi hivyo hatari kumewafanya maafisa nchini humo kuweka hali ya tahadhari nchini nzima. 

Wasiwasi wa idadi ya maambukizi kuongezeka umekumba nchi nyingi za Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles