26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwinyi aahidi kuboresha mazingira ya walimu Z’bar

Na MWANDISHI WETU -ZANZIBAR

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema akipata ridhaa ya wa- nanchi, Serikali atakayoiongoza itahakikisha inaboresha mazin- gira ya walimu.

Dk. Mwinyi alisema Seri- kali atakayoiongoza itaboresha mazingira kwa walimu ikiwemo kuwapandisha madaraja na kuongeza posho kwa walimu wakuu.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati akizungumza na walimu wa shule za msingi na sekondari mjini Unguja, ikiwa ni mwende- lezo wa ziara zake za kukutana na makundi mbalimbali.

“Sioni tatizo kuongeza posho kwa walimu wakuu hawa kama Serikali itakuwa na uwezo wa fedha.

“Kwa mujibu wa taarifa za Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU), inaonyesha ombi hili lilikuwa limekubalika, lakini utekelezaji wake ulikuwa bado

kutokana na Covid-19, hivyo ni- talishughulikia,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema pia Serikali yake itahakikisha inawapandisha ma- daraja walimu na kwamba ni jambo muhimu sana.

“Suala la kuwepo tume ya utumishi wa walimu ndiyo lita- fanya kazi vizuri, haiwezekani mwalimu aliyefanya kazi miaka 10 anaingia mwingine kijana leo anakuwa sawa sawa kwa kila kitu,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema suala la walimu ku- tolipwa posho zao kwa wakati wanapokwenda safari za kikazi katika maeneo ya Unguja na Pemba amelipokea na atalifanyia kazi akipata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar.

Alisema ataiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ku- kutana mara kwa mara na chama cha walimu angalau mara mbili kwa mwaka.

“Ninapowateua watendaji ambao hawakutani na watu wa- naowaongoza, kiukweli utakuwa huongozi sababu hatakuwa ana- fanya mambo anayoyataka yeye,

wadau hujui wanataka nini, yaani mara mbili kwa mwaka kuna uku- bwa gani, sasa haya tutayaweka sawa na mrejesho ufike kwa rais,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema kuhusu suala la mikopo ya elimu ya juu kwa wal- imu amelipokea na kwamba kuna haja ya kuhakikisha walimu wal- ioajiriwa wanapewa mikopo hiyo ikilinganishwa na ilivyo sasa am- bapo wanapewa wasioajiriwa.

“Mimi kwa maoni yangu ni- takaowateua katika nafasi nita- hakikisha wanafanya mapitio ya sheria na sera za elimu ili kuleta tija kwenye sekta hii muhimu.

“Sheria hii ya elimu imepitwa na wakati ambapo ni ya mwaka 1982 na imepitiwa mwaka 1986, hivyo kuna mambo yatakuwa yamepitwa na wakati lazima ya- fanyiwe marekebisho,” alisema Dk. Mwinyi.

Katibu Mkuu wa ZATU, Mus- sa Omar Tafurwa alisema kuna haja ya Serikali atakayoiongoza ihakikishe inapitia upya sera ya elimu ambayo ilipitiwa mwaka 2006.

Alisema kuanzia mwaka huo

ambao sera hiyo imepitiwa na kuanza kutumika mwaka 2010, hadi sasa kuna maeneo ambayo yametekelezwa na kuna maeneo hayajatekelezwa na kuna maeneo ambayo si mwafaka kwa sasa.

“Moja ya kilio cha muda mrefu kwa walimu Zanzibar ni upandishwaji wa madaraja ya kiutumishi, kuna wakati miaka minne iliwahi kutoka barua Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, lakini ikaonekana kuna mapungufu na hatimaye zikaf- utwa barua hizo zote, sasa ma- daraja yanajenga heshima, hivyo tunaomba walimu tupandishwe daraja,” alisema Tafurwa.

Alisema jambo lingine amba- lo walimu wanaomba ni kupewa bima ya afya kwa sababu ghara- ma za huduma za matibabu ya afya zinawasumbua sana walimu.

Rais wa ZATU, Seif Moham- ed Seif alisema ualimu imekuwa ni miongoni mwa kazi ambazo zimekuwa zikidhalilishwa na kwamba kuna haja ya kuhakiki- sha masilahi ya walimu yanazingatiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles