26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Msami awaomba wananchi wasifanye makosa Oktoba 28

Mwandishi Wetu

Mwanaharakati wa kupigania haki katika jamii Mathew Msami, amewaomba wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi wenye lengo la kuiletea nchi maendeleo na sio wenye kutaka kujinufaisha wenyewe.

Akizungumza na MTANZANIA mapema leo jijini Dar es Salaam, Msami, amesema nchi imefikia hapa ilipo kutokana na uongozi bora wa Dkt John Magufuli kwa kupigania misingi imara.

Anasema wananchi wanatakiwa wasifanye makosa katika kulitambua hili na kutofanya makosa kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu. 

“Dk. Magufuli katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake alitumia vizuri uongozi kwaajili ya kuiletea nchi manufaa na sio kujinufaisha,  kwa kuwa amefanya mengi ambayo hayaitaji kuambiwa leo hii Dar es Salaam yetu kama nchi za wenzetu huko nchi za nje, tunapita barabara za juu, madaraja ya kisasa na mambo mengi ambayo tunajivunia nayo” anasema Msami.

Anasema miundombinu mizuri ambayo imetekelezwa na uongozi wa serikali ya CCM imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato kutokana na wananchi kutotumia muda mwingi barabarani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles