Msanii huyo alifariki Januari 10 mwaka huu, baada ya kuugua kwa miezi 18 kutokana na saratani na albamu yake iliwekwa sokoni Januari 8.
Black Star ndiyo albamu ya kwanza nchini Marekani kuuza sana baada ya albamu ya marehemu Michael Jackson, ambaye alitamba na albamu yake ya ‘This is it’, iliyoongoza katika mauzo Novemba mwaka 2009.
Albamu nyingine za Bowie pia ziliorodheshwa miongoni mwa albamu 200 za Billboard wiki hii, huku albamu ya ‘The best of Bowie’ ikishika nafasi ya nne na ‘The Rise and Fall of Ziggy Stardust’ na ‘Spiders from Mars’ zikishikilia nafasi ya 21.