Johannesburg, Afrika Kusini
Wanafunzi wa Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa fainali za Mashindano ya kimataifa ya TEHAMA kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara yanayoandaliwa na Huawei chini ya kaulimbiu ya “Connectivity, Glory, Future”.
Kwa mwaka jana wanafunzi kutoka Tanzania na Nigeria walikuwa washindi wa jumla katika shindano hilo na hivyo kuwakailisha ukanda huo katika mashindano ya dunia.
Shindano hilo lilizinduliwa jijini Johannesburg, Africa Kusini juzi Septemba 10, katika hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao, shindano hilo linaaminika kuwa ndiyo kubwa zaidi la aina yake barani Afrika kwa kushirikisha nchi 14 na kuhushisha wanafunzi zaidi ya 50,000.
Shindano la TEHAMA linaloandaliwa na Huawei, kwa mwaka huu limeshirikisha zaidi ya nchi 70 Ulimwenguni kote, na kushindanisha wanafunzi 150,000 kutoka vyuo zaidi ya 2000.
Tangu kuzinduliwa kwake miaka mitano iliyopita, Shindano la TEHAMA la Huawei limeendelea kukua na kuwa shindano kubwa Zaidi la TEHAMA barani Africa.
Katika uzinduzi uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano, UNESCO pamoja na wanafunzi, Makamu Rais wa Huawei Afrika Kusini, Liao Yong alielezea umuhimu wa mawasiliano katika zama hizi za kutokusogeleana.
“Utofauti katika mapokeo ya kidigitali unazidi kuongezeka katika kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na janga la Covid-19. Wakati watu wanapojisomea na kufanya kazi mtandaoni, wale wenye changamoto za kidigitali wanaathirika zaidi”. Alisema Liao.
Katika semina ya mtandaoni iliyoandaliwa na UNESCO buni hivi kari, ilibainishwa kuwa miundombinu ya kidigitali ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili sekta ya elimu ya juu barani Afrika