Asha Bani-Dar es Salaam
Shirika lisilo la kiserikali la Paradigm Initiative Afrika limewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria, waandishi wa habari na walimu kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Majadiliano hayo yamehusisha nchi za Afrika ya Kati ikiwemo Nigeria ambapo wadau wa mitandao kutoka katika nchi hiyo walishiriki kikamilifu pamoja na kutoa maoni yao kwa njia ya mtandao walitamani kupata uzoefu kutoka Tanzania ambayo tayari imepiga hatua ikiwemo kudhibiti kikamilifu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Pamoja na mambo mengine wadau hao wamepata nafasi ya kuangalia na kujadili muswada wa Nigeria unaohusu masuala ya matumizi ya mtandao pamoja na kuangalia ni maeneo gani ya kusaidia kuboresha ufanisi pamoja na misingi bora ya utumiaji ya mitandao ya kijamii kwa Tanzania na Afrika ya sasa kwa siku za baadae.
Mdau na mtumiaji wa mtandao ambaye pia ni Mratibu wa majadiliano hayo, Peter Mmbando amesema ni wakati mwakafa wa kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na nchi nyingine ili kuona nini cha kujifunza kuendana na wakati kwa mahitaji ya sasa na baadae.
Aliwahisi watumiaji wa mtandao kuendelea kufuata sheria zilizopo ili kuendana na mahitaji ya sasa .