26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Benki ya PBZ yaahidi kuendelea kutoa mikopo kwa wakulima

HADIJA OMARY LINDI

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), imesema itaendelea kuwaunga mkono wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara  moja kwa moja katika kuwapa mikopo ya pembejeo.

Hayo yameelezwa na Ofisa masoko wa benki hiyo, Nasoro zaid alipokuwa  akizungumza na Mtanzania Digital juu ya namna Benki hiyo inavyoshiriki katika kuwasaidia wakulima wa mkoa huo katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya Kusini  katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi yanayoendelea hivi sasa.

Zaid amesema kwa kutambua shuguli zinazofanywa na wakulima benki hiyo imeamua kutoa mikopo ya pembejeo na matrekta kwa wakulima yenye lengo la kuwasaidia kuongeza tija ya uzalishaji katika kilimo chao.

Amesema kwa mwaka 2018/19 benki yao imewakopesha wakulima fedha  zaidi ya bilioni nne kwa ajili ya kununua pembejeo za kilimo pamoja na maandalizi ya mashamba ambapo kwa mwaka huu tayari imekopesha shilingi bilioni moja na kuongeza kuwa mikopo hiyo inaongezeka ama kupungua kulingana na mahitaji ya wakulima katika msimu wa mazao husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles