26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mmisionari akiri makosa ya unyanyasi kingono

WASHINGTON, Marekani

MMISHONARI Mkristo wa raia wa Marekani, amekiri mahakamani makosa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wasichana wadogo katika makao ya mayatima alioanzisha nchini Kenya.

Gregory Dow (61), alikubali makosa manne dhidi yake ya kujihusisha na tabia ya unyanyasaji wa kingono na watoto wadogo nchi ya kigeni.

Makao ya watoto mayatima yalikuwa yanatoa huduma kuanzia  mwaka 2008 hadi  Dow alipoondoka Kenya na kurejea kwao Marekani.

Shirika la Upelelezi Marekani (FBI) na mamlaka ya Kenya, zilimchunguza mtuhumiwa na akafikishwa mahakamani nchini Marekani.

Mwaka 2008, Dow alianzisha makao ya yatima magharibi mwa Kenya. Makao hayo pia yalikuwa yanasimamiwa kwa pamoja na makanisa kaunti ya Lancaster jimbo la Pennsylvania, nchini Marekani kulingana na gazeti la eneo la LNP.

Alishtumiwa kwa kunyanyasa wasichana kuanzia mwaka 2013. Wasichana wawili kati ya walionyanyaswa walikuwa na umri wa miaka 11, mmoja miaka 12 na mwingine miaka 13, gazeti la ALP limeongeza.

“Mshtakiwa alijifanya kuwa mmishonari mkristo aliyejali watoto hao na kuwataka wamuite ‘Baba’. Hata hivyo, badala ya kuchukuwa majukumu ya baba, aliwanyanyasa ujana wao na kutumia vibaya hali yao ya kutojiweza,” imesema Idara ya Sheria ya Marekani katika taarifa yake.

Alitoroka Kenya, Septemba, 2017, baada ya kuibuka kwa madai ya unyanyasaji, taarifa hiyo imeongeza.

“Gregory Dow kwa upande mwingine, alificha uovu aliokuwa nao katika imani yake, akiwa na matumaini kwamba nchini Marekani hakuna atakayejua anachofanya au kutunza watoto aliowanyanyasa. Alifanya makosa,” Wakili William McSwain wa Marekani alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles