30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Azaliwa na jinsi mbili

NAIROBI, Kenya 

KILA anapofikiria kutangamana na watu wanaoifahamu hali yake, Sidney Etemesi anaanza kuishiwa na nguvu na ujasiri hata wa kutembea au kutoka nje.

Etemesi ni Mkenya aliyezaliwa akiwa na viungo vya uzazi aina mbili, uume na uke.

Maumbile yake yamekuwa changamoto kubwa katika uhusiano wake na watu wengine katika jamii. 

Kila siku, ameishi kukejeliwa kushoto kulia na wanaofahamu hali yake, japo si ya kujitakia.

Kwa  kwa kumwangalia tu, bila kujua hali yake ya kuzaliwa nayo, basi utamfananaisha na mtu wa kawaida tu.

Yeye huishi kama mwanamume ingawa kwa kiasi muonekano wake wa sura unaegemea upande wa wanawake.

Ni hali ambayo humchanganya Sidney kila kuchao, anapopambana na nafsi yake na kujaribu kujitambulisha kwa wengine.

“Kila siku ya maisha yangu, ninapoingia kwenye bafu nikijitazama maumbile yangu ya kuwa na uke na uume katika mwili mmoja huwa najihisi mnyonge na mwenye hofu kuu. Ila sina lakufanya,” anasema Sydney.

Sidney alizaliwa akitambulika kama binti au msichana, na wazazi wake wakampa jina Beatrice .

Malezi ya Sydney yalikuwa kama ya watoto wengine kwa kuwa hali yake ya maumbile ilikuwa ni siri iliyokuwa imefichwa sana na wazazi wake.

Binafsi hakuwa na ufahamu kuwa alikuwa tofauti na watoto wengine na wala hakuwa na ufahamu kuwa maumbile ya kawaida huwa binadamu anabeba aina moja tu ya viungo vya uzazi.

Lakini siku zilivyozidi kusonga, alianza kujihisi ndani yake kwamba anavutiwa na kukumbatia tabia za kiume. Alianza kujitambulisha kama mtoto wa kiume na kutaka kucheza na wavulana. Lakini hapo ndipo matatizo kati yake na wazazi wake yalipoanza.

Wazazi wake hawakumuunga mkono, wala hawakutaka kusikia chochote kuhusu zisia zake. Walichofahamu ni kuwa mtoto wao alikuwa binti na hakukuwa na cha ziada.

Matatizo zaidi yalianza pale alipoanza kubalehe akiwa na umri wa miaka 13. Mwili wake ulianza kubadilika kama wanarika wengine, japo mabadiliko yake yalianza kufanana na yale ya kiume.

“Nilichukua uamuzi wa kujitambulisha kama mwanamume kwa kuwa mwili ndio uliokuwa unanielekeza. Homoni za mwili wangu zilinielekeza hivyo” Sidney alisema

Alipochukua uamuzi huo mambo yakaenda mrama zaidi. Alitengwa na hatimaye kufukuzwa nyumbani.

Alibaguliwa na kuchekwa kwa kujitambulisha kama mwanamume ilhali muonekano wake wa sura ulikuwa wa kike .

“Muonekano wangu bila shaka umekuwa ukiwakanganya watu sana. Sura yangu na maumbile yangu ya nje ya mwili yana muonekano wa kike zaidi. Lakini undani wangu hisia zangu na nguvu zangu nazihisi kama za kiume tangu zamani,” anasema Sydney.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles