27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yatoa sababu za kulipua ofisi

KAESONG, Korea Kaskazini

KOREA Kaskazini, imeelezea kwanini iliamua kulipua ofisi ya pamoja katika mji wa Kaesong.

Taarifa iliyotolewa na  Korea Kaskazini imeishtumu Korea Kusini kwa kuvunja makubaliano yao ya  mwaka 2018 na kuonesha tabia za kama “mbwa koko”, huku dada yake kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini akimshtumu Rais wa Korea Kusini kwa kuwa kibaraka wa Marekani.

Wakati huohuo, Waziri wa Korea Kusini wa Uhusiano wa Masuala ya Nchi hiyo na Korea Kaskazini, ameandika barua ya kujiuzulu, baada ya uhusiano wa nchi hizo mbili kuzorota zaidi.

Hatua hiyo inawadia baada ya Korea Kaskazini kulipua ofisi ya pamoja ya nchi hizo mbili za Korea iliyokuwepo mpakani ambayo ilijengwa kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Wakati huohuo, jeshi la Korea Kaskazini, limesema  litatuma wanajeshi wake  maeneo yasioruhusiwa vita kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.

Upande wa Korea Kusini, nayo imekuwa ikiendelea kusema iko tayari kwa mazungumzo, lakini imeishitumu Korea Kaskazini na kutaja vitendo vyao kama watu wasio na akili na vyenye kusababisha uharibifu zaidi.

Katika wiki za hivi karibuni, wasiwasi umekuwa ukiendelea kuongezeka  kwa kiasi fulani, ukisemekana kuchochewa na raia wa Korea Kaskazini waliotoroka Korea Kusini ambao wanapinga serikali kwa kuendeleza propaganda zao kupitia mpaka wa nchi hizo mbili.

Chombo cha habari cha Korea Kaskazini kinachomilikiwa na Serikali, kimeshtumu Korea Kusini kwa kuvunja makubaliano ya 2018, ikiwemo azimio la Panmunjom.

Taaifa hiyo ilimfananisha waziri wa ulinzi wa Korea Kusini na “mbwa koko muoga” ambaye anajiona mwenye fahari na jasiri, anayepindainda mazungumzo na mshirika mwenzake na kuchochea mazingira ya kuzozana.

Wakati huohuo, jeshi la Korea Kaskazini limesema itapeleka wanajeshi walke katika eneo kulikokuwa na ofisi ya ushirikiano kwa pande hizo mbili mji wa kiviwanda wa Kaesong na mlima Kumgang – eneo la kitalii mashariki mwa pwani.

Kim Yo-jong – dada yake kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un – alimshambulia Rais wa Korea Kusini kwa maneno.

“Sababu kutofanikiwa kwa makubaliano mazuri ya kaskazini na kuzini – ambayo hayakutekelezwa hata chembe ni kibaraka wa Marekani.”

“Hata kabla ya wino wa makubaliano ya kaskazini na kusini kukauka, alikubali ‘ushirikiano wa kikazi wa Korea Kusini -Marekani’ chini ya shinikizo la mkuu wake.

Taarifa hiyo inawadia baada ya dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kusini Jumamosi.

“Msimamo wetu ni kuwa makubaliano ya kijeshi ya Septemba 19, yanastahili kutekelezwa bila pingamizi lolote kwa misingi ya kupatikana kwa Amani katika rasi ya Korea na kuzuia migogoro,” alisema Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles