32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kahata: Kiwango Simba bado kabisa

ZAINAB IDDY- DAR ES SALAAM

KIUNGO wa Simba, Francis Kahata, amesema licha ya kila mchezaji wa timu hiyo kujituma mazoezini na katika mechi za kirafiki, lakini bado hawajafikia kiwango ambacho walikuwa nacho kabla ya kusimama kwa Ligi Kuu.

Machi 17 mwaka huu, Serikali ilipiga marufuku mikusanyiko ikiwemo michezo kwa siku 30 kabla ya kurefusha katazo hilo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vya corona ambao vimeitikisa dunia huku vikisababisha vifo vya maelfu ya watu.

Uamuzi huo wa Serikali ulisababisha Shirikisho la Soka Tanzania( TFF), kusimamisha ligi zote inazozisimamia ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, uamuzi uliozifanya klabu pia kuwapa mapumziko wachezaji wao.

Lakini baada ya hali ya mambo kuendelea kuwa shwari Rais John Magufuli aliruhusu shughuli za michezo kuendelea ikiwemo ligi kuanzia Juni Mosi, ambapo sasa Ligi Kuu imepangwa kuendelea Juni 13.

Kahata aliliambia MTANZANIA jana kuwa, kabla ya ligi kusimama kila mchezaji katika kikoci chao alikuwa bora kiasi cha kuwepo kwa presha miongoni mwao juu ya kupata nafasi ya kuanza.

“Kwa sasa nitofauti kwa sababu ukiangalia unajua wachezaji hawa lazima waanze kutokana viwango vyao kitu ambacho awali hakikuwepo, wote walikuwa na viwango vya kufanana na hivyo kutoa ugumu katika kupanga kikosi.

“Ni kweli tumecheza mechi za kirafiki asubuhi na jioni na zote tumeshinda, lakini ninachoona ni kwamba wachezaji bado hatujafikia kwenye ule ubora ambao tuliishia nao kabla ya janga hili, lakini taratibu tunaanza kurejea kikubwa ni sisi kuendelea kufuata kile tunachoambiwa na walimu” alisema Kahata

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles