27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Eymael:Nimerudi Yanga na nguvu mpya

Mwamvita Mtanda ,Dar es Salaam

BAADA ya Sintofahamu ya takaribani wiki tatu kuhusu kurejea kwa kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, hatimaye amewasili jana na atajiunga na kikosi chake leo.

Eymael  hataki kupoteza muda , leo hii ataondoka na ndeki ya Shirika la Precision, kulekea Sinyanga  kukutana  wachezaji wake, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Mwadu.

Licha ya kuwa Mbelgiji huyo alitua   saa 1:30 na Ndege ya Shirika la Ethiopia, lakini  uongozi wa Yanga amempotezea na hakuna hata mmoja aliyefika kumpokea.

Akizungumza  na MTANZANIA  jana, baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere, Eymael alisema, jambo la kushukuru kwake ni kuwa amerudi salama na kuwahi  mechi yao na  Mwadui.

Alipoulizwa kuusu kutopokelea na uongozi wa Yanga, Mbelgiji huyo alisema,  hakutarajia kama wasingekuja kumpokea lakini inawezekana wamebanwa na majukumu mengine, lakini  ataweza kufika nyumbani kwake.

“Siwezi kufahamu kwanini hawakuja, lakini kila jambo linakwenda kwa ratiba, yawezekana wamebanwa lakini haiweze kufanya nisifike nyumbani.

“Nimepambana sana kurudi niwahi kazi yangu, pia kuona wachezaji wangu wakiwa uwanjani  Jumamosi, siwazi mengine, nawaza kufanya kazi  yangu iwe nzuri  hasa  majukumu tuliyonayo,”alisema Eymael.

Eymael alisema amerudi na nguvu  mpya kuhakikisha kuwa timu yake inafanikiwa kufanya vyema, hasa katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, pia kumaliza  Ligi katika nafasi ya pili ambayo itawawezesha kushiriki michuano ya  shirikisho ya kimataifa.

Mbelgiji huyo aliongeza kuwa, ataanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi chake akifika Shinyanga, ambapo  ataongoza mazoezi  ya asubuhi  Ijumaa asubuhi.

MTANZANIA  lilimsaka, Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli, ili kufahamu  sababu iliyowakwamisha kuja kumpokea Kocha wao.

Bumbuli alisema, hakukuwa na ulazima wa wao kwenda kumpokelea, kwa kuwa kocha huyo tayari anayafahamu mazingira ya Tanzania, hasa kutoka uwanjani wa ndege hadi nyumbani kwake Mikocheni.

“ Sioni kama kuna tatizo  eti hakuja kupokelewa, sio mgeni anapafahamu kwake, hivyo tulikuwa tunaamini angeweza kufika,”alisema Bumbuli.

Kocha huyo alitua na mabagi  matano ya vifaa mbali mbali vya michezo, baada ya kuona mapunguvu katika vifaa wanavyotumia sasa.

Pia Mbelgiji huyo aliambatana na  mke wake, Patricia Abbruzzesse Eymael, ambaye alifunga naye ndoa hivi karibuni.

“Nafurahi sana kuja Tanzania  nikiwa nimeambatana na mume wangu, mimi nishabiki wa Yanga, naisapoti pia namsapoti Eymael afanye kazi nzuri.

Natamanini tuishi sana Tanzania, lakini inategemea na mkataba wake na Yanga kama utaendelea itakuwa furaha zaidi kwetu,”alisema Patricia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles