27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

LSF yatoa ripoti ya upatikanaji haki za kisheria

Mwandishi wetu -Dar es salaam

SHIRIKA lisilo la kiserikali linaloshughulika na uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria, kupitia wasaidizi wa kisheria nchini, Legal Services Facility (LSF), ambalo linakuza na kulinda haki za binadamu hasa kwa wanawake masikini na makundi mengine, limefanya tathmini na kutoa ripoti ya upatikanaji wa haki za kisheria iliyotekelezwa tangu mwaka 2016.

Ripoti hiyo inatoa tathmini ya awamu ya pili ya programu ya miaka mitano inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Denmark (Danida), Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) kupitia mfuko wao wa maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ngw’anakilala alisema kuwa progamu ya utekelezaji wa upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria imekuwa na mafanikio makubwa katika kuunganisha utamaduni wa kutafuta kurekebisha masuala ya kisheria katika jamii hasa kwenye masuala ya kisheria na haki za binadamu.

Alisema kuwa kuna makubaliano muhimu na wadau ya kuwa na msaada wa kisheria kwa kuboresha masuala muhimu tangu kuanza kwa utekelezaji wa programu hiyo, ambayo hutolewa kwa mfumo wa huduma za msaada wa kisheria na katika kila wilaya nchini.

“Kiini cha programu ni kutaka kujibu ajenda ya kitaifa iliyopo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Ngw’anakilala.

Alisema kuwa licha ya hali hiyo programu hiyo inaendana na mfumo wa kitaifa kama vile sheria ya msaada wa kisheria ya mwaka 2017, mpango wa taifa wa kumaliza unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa 2017/18-2021/22  pamoja na sera ya masuala ya jinsia.

Ngw’anakilala, alisema kuwa LSF inathamini uhusiano uliopo na Serikali kupitia wizara kama vile Tamisemi, Wizara ya Afya na Wizara ya Sheria kwa pande zote za Muungano.

 “Jukumu letu ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuweka mazingira ya upatikanaji wa haki na sheria kama kichocheo muhimu cha maendeleo nchini.

“Wadau wetu katika utekelezaji huu wamekubali kuwa kuna uhusiano mzuri na ushirikiano kati ya watendaji wa Serikali katika kiwango cha mikoa na katika halmashauri,” alisema Ng’wanakilala.

Kwa upande wake Meneja wa Ufuatiliaji, Matokeo na Tathmini wa LSF, Said Chitung alisema kuwa miongozo ya mahojiano ilitengenezwa kwa makundi maalumu kutoka katika kiwango cha chini cha jamii.

Alisema watoa taarifa kutoka katika jamii ya chini walichaguliwa kimkakati kutoka katika kata kwenye wilaya kwenye mikoa 28 ya Tanzania bara na visiwani ambapo watoa habari 287 walihojiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles