26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

LIGI KUU BARA KUPIGWA NYUMBANI, UGENINI

 ZAINAB IDDY -DAR ES SALAAM 

RASMI sasa mechi zote za Ligi Kuu Tazanzania Bara, zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini bila kuwapo vituo kama ilivyoelekezwa awali. 

Ligi za Tanzania zinatarajiwa kurejea kuanzia Juni 13, mwaka huu baada ya Serikali kuruhusu kuendelea kuanzia leo kutokana na kupungua kwa kasi ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya. 

Awali, Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya michezo, ilitangaza ligi zingechezwa katika vituo viwili, Dar es Salaam (Ligi Kuu na Kombe la FA) na Mwanza Daraja la Kwanza na la Pili). 

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr. Hassan Abbas, alisema kutokana na hali kuwa shwari, Serikali imeridhia ligi kuchezwa kama ilivyokuwa awali. 

Abbas alisema kuwa suala hilo limezingatia maoni ya Wizara ya Afya pamoja na wadau 

 mbalimbali wa masuala ya michezo nchini.

“Serikali imeridhia mfumo wa michezo ya soka ichezwe kama ilivyokuwa ukifanyika awali, yaani kwa mfumo wa nyumbani na ugenini, kabla ya virus vya corona.

“Awali, ilipangwa ichezwe kwa vituo na ilitokana na kuwepo kwa virus vya corona, lakini kwa kuwa hali inazidi kuwa shwari, Serikali imeridhia kuwe na mechi za nyumbani na ugenini kwa kila mechi ili kutoa burudani na furaha iendelee vilevile,” alisema.

Aliongeza: “Jambo la msingi ni kuona utaratibu unafuatwa ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya virus vya corona kwani licha ya kwamba hali imekuwa shwari, ni lazima kuchukua tahadhari.”

Wakati huo huo, Abbas, amesema ligi zitakapoanza, mashabiki ni ruksa kwenda viwanjani, lakini kwa kuzingatia mwongozo ambao umetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya.

“Serikali imeridhia mashabiki watakaotaka kwenda uwanjani wanaruhusiwa kwenda kama utaratibu ulivyokuwa awali, kabla ya virus vya corona, pia nyingine zitaonyeshwa ‘live’ kama kawaida, lakini lazima wafuate mwongozo na kuchukua tahadhari dhidi ya corona.

 “Kila uwanja, shabiki atapimwa joto na kwa upande wa mechi kubwa ambazo zitahusisha mashabiki wengi na kuleta changamoto kwa upande wa mita moja, maelezo ni kuwa wataingia nusu ya wanaotakiwa kuingia uwanjani.”

Awali, Serikali ilitoa taarifa kwamba mashabiki watakaoruhusiwa kwenda uwanjani ni 20 ambapo kila timu ingetoa mashabiki 10 pekee ili kuchukua tahadha 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles