*Amzidi kete kidiaba na kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika
ABUJA, Nigeria
MSHAMBULIAJI raia wa Tanzania anayehusishwa kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Ally Samatta, ameweka historia ya kuwa Mtanzania ya kwanza kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani.
Katika tuzo hizo zilizofanyika jana usiku jijini Abuja, Nigeria, Samatta aliwabwaga mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mshambuliaji raia wa Algeria anayekipiga kwa mkopo Etoile du Sahel ya Tunisa akitokea Al Sadd ya Qatar, Baghdad Boundjah.
Samatta ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa nchini Nigeria, alikua na mchango mkubwa katika klabu yake ya TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika mwaka jana.
Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars aliifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao saba sawa na mshambuliaji wa El Merrikh ya Sudan, Bakri Al-Madina, na kuibuka kinara wa mabao.
Pierre-Emerick Aubameyang, raia wa Gabon anayekipiga Borussia Dortmund ya Ujerumani alitangazwa Mwanasoka Bora wa Afrika 2015 na kuzima ndoto za kiungo wa Manchester City ya England na raia wa Ivory Coast, Yaya Toure, kutwaa tuzo hiyo kwa mwaka wa tano mfululizo.
Nafasi ya tatu katika tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika ilimwendea mshambuliaji wa Swansea City ya England raia wa Ghana, Andre Ayew.
Washindi wa tuzo mbalimbali za mwaka kwa mabano ni Victor Osimhen (chipukizi bora), Herve Renard (kocha bora), Bakary Gassama (refa bora), Ivory Coast (timu bora ya taifa), TP Mazembe (klabu bora), Cameroon (timu bora ya taifa ya wanawake), Oghenekaro Etebo (kipaji cha mwaka) na Gaëlle Enganamouit (mwanasoka bora wa kike).
Mwanasoka Bora Afrika
2015 Â Â Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)
2014 Â Â Yaya Toure (Ivory Coast)
2013 Â Â Yaya Toure (Ivory Coast)
2012 Â Â Yaya Toure (Ivory Coast)
2011 Â Â Yaya Toure (Ivory Coast)
2010 Â Â Samuel Eto’o (Cameroon)
2009 Â Â Didier Drogba (Ivory Coast)
2008 Â Â Emmanuel Adebayor (Togo)
2007 Â Â Frederic Kanoute (Mali)
2006 Â Â Didier Drogba (Ivory Coast)
2005 Â Â Samuel Eto’o (Cameroon)
2004 Â Â Samuel Eto’o (Cameroon)
2003 Â Â Samuel Eto’o (Cameroon)
2002 Â Â El Hadji Diouf (Senegal)
2001 Â Â El Hadji Diouf (Senegal)
2000 Â Â Patrick Mboma (Cameroon)
1999 Â Â Nwankwo Kanu (Nigeria)
1998 Â Â Mustapha Hadji (Morocco)
1997 Â Â Victor Ikpeba (Nigeria)
1996 Â Â Nwankwo Kanu (Nigeria)
1995 Â Â George Weah (Liberia)
1994 Â Â Emmanuel Amunike (Nigerua)
1993 Â Â Rashid Yekini (Nigeria)
1992 Â Â Abedi Pele (Ghana)
Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani
2015   Mbwana Samatta (Tanzania – TP Mazembe)
2014 Â Â Firmin Ndombe Mubele (DR Congo – Vita Club)
2013 Â Â Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)
2012 Â Â Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)
2011   Oussama Darragi (Tunisia – Espérance)
2010 Â Â Ahmed Hassan (Misri – Al-Ahly)
2009   Tresor Mputu (DR Congo – TP Mazembe)
2008 Â Â Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)
2007   Amine Chermiti (Tunisia – Étoile du Sahel)
2006 Â Â Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)
2005 Â Â Mohamed Barakat (Misri – Al-Ahly)