31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Viva samatta

*Amzidi kete kImageidiaba na kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika

ABUJA, Nigeria

MSHAMBULIAJI raia wa Tanzania anayehusishwa kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Ally Samatta, ameweka historia ya kuwa Mtanzania ya kwanza kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani.

Katika tuzo hizo zilizofanyika jana usiku jijini Abuja, Nigeria, Samatta aliwabwaga mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mshambuliaji raia wa Algeria anayekipiga kwa mkopo Etoile du Sahel ya Tunisa akitokea Al Sadd ya Qatar, Baghdad Boundjah.

Samatta ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa nchini Nigeria, alikua na mchango mkubwa katika klabu yake ya TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika mwaka jana.

Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars aliifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao saba sawa na mshambuliaji wa El Merrikh ya Sudan, Bakri Al-Madina, na kuibuka kinara wa mabao.

Pierre-Emerick Aubameyang, raia wa Gabon anayekipiga Borussia Dortmund ya Ujerumani alitangazwa Mwanasoka Bora wa Afrika 2015 na kuzima ndoto za kiungo wa Manchester City ya England na raia wa Ivory Coast, Yaya Toure, kutwaa tuzo hiyo kwa mwaka wa tano mfululizo.

Nafasi ya tatu katika tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika ilimwendea mshambuliaji wa Swansea City ya England raia wa Ghana, Andre Ayew.

Washindi wa tuzo mbalimbali za mwaka kwa mabano ni Victor Osimhen (chipukizi bora), Herve Renard (kocha bora), Bakary Gassama (refa bora), Ivory Coast (timu bora ya taifa), TP Mazembe (klabu bora), Cameroon (timu bora ya taifa ya wanawake), Oghenekaro Etebo (kipaji cha mwaka) na Gaëlle Enganamouit (mwanasoka bora wa kike).

Mwanasoka Bora Afrika

2015    Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)

2014    Yaya Toure (Ivory Coast)

2013    Yaya Toure (Ivory Coast)

2012    Yaya Toure (Ivory Coast)

2011    Yaya Toure (Ivory Coast)

2010    Samuel Eto’o (Cameroon)

2009    Didier Drogba (Ivory Coast)

2008    Emmanuel Adebayor (Togo)

2007    Frederic Kanoute (Mali)

2006    Didier Drogba (Ivory Coast)

2005    Samuel Eto’o (Cameroon)

2004    Samuel Eto’o (Cameroon)

2003    Samuel Eto’o (Cameroon)

2002    El Hadji Diouf (Senegal)

2001    El Hadji Diouf (Senegal)

2000    Patrick Mboma (Cameroon)

1999    Nwankwo Kanu (Nigeria)

1998    Mustapha Hadji (Morocco)

1997    Victor Ikpeba (Nigeria)

1996    Nwankwo Kanu (Nigeria)

1995    George Weah (Liberia)

1994    Emmanuel Amunike (Nigerua)

1993    Rashid Yekini (Nigeria)

1992    Abedi Pele (Ghana)

 

Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani

2015    Mbwana Samatta (Tanzania – TP Mazembe)

2014    Firmin Ndombe Mubele (DR Congo – Vita Club)

2013    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2012    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2011    Oussama Darragi (Tunisia – Espérance)

2010    Ahmed Hassan (Misri – Al-Ahly)

2009    Tresor Mputu (DR Congo – TP Mazembe)

2008    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2007    Amine Chermiti (Tunisia – Étoile du Sahel)

2006    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2005    Mohamed Barakat (Misri – Al-Ahly)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles