27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta arudi mazoezini Aston Villa

LONDON, ENGLAND 

MSHAMBULIAJI wa timu ya Aston Villa, Mbwana Samatta, ameungana na wachezaji wengine watatu wa timu hiyo na kufanya mazoezi ya pamoja.

Mbali na Samatta, wachezaji wengine ambao ameungana nao ni pamoja na Ahmed Elmohamady, Marvelous Nakamba pamoja na Trezeguet.

Mazoezi ya timu hiyo yalianza tangu Jumatano baada ya shirikisho la soka nchini England kutangaza timu zote zianze mazoezi kwa ajili ya kuendelea na michezo iliyosalia ya Ligi Kuu msimu wa 2019/2020.

Samatta yeye aliungana na wachezaji hao siku ya Ijumaa, lakini wachezaji wengine wanne walianza tangu Jumatano baada ya uongozi wa timu hiyo kuwafungulia milango wachezaji wake kuanza mazoezi.

Wakati wa mazoezi hayo bado walionekana kufuata utaratibu wa kukaa mbalimbali bila ya kugusana, huku kocha wao Dean Smith akiwa amevaa barakoa.

Ligi mbalimbali duniani zilianza kusimama tangu Machi mwaka huu kutokana na kuenea kwa homa ya mapafu ambayo inasababishwa na virusi vya corona. Virusi hivyo vimepoteza idadi kubwa ya watu na wengine wakipata maambukizi.

Ligi ya England inatarajia kurejea Juni 12 mwaka huu ili kumalizia michezo hiyo iliyobaki, lakini itapigwa bila ya mashabiki viwanjani kwa kuhofia kuenea kwa virusi hivyo.

Wiki moja iliyopita wachezaji wote wa ligi hiyo pamoja na viongozi wa klabu walifanyiwa vipimo kwa ajili ya kujihakikishia usalama wao.

Aston Villa wao wapo katika hali ngumu ya kushuka daraja huku wakiwa nafasi ya 19 baada ya kucheza michezo 28 na kujikusanyia pointi 25.

Samatta anaangaliwa kwenye kikosi hicho kwa kushirikiana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kuipigania timu hasa kwa upande wake katika nafasi ya ushambuliaji.

Hadi sasa ana jumla ya mabao mawili aliyoyafunga katika michezo sita aliyocheza kwenye michuano mbalimbali tangu ajiunge na klabu hiyo wakati wa Januari akitokea klabu ya Genk.

Nahodha hiyo wa timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars, alifunga bao lake la kwanza kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Bournemouth, Februari 1 huku bao la pili akifunga dhidi ya Man City kwenye fainali ya Kombe la Ligi, Machi 1, huku Aston Villa wakipoteza kwa mabao 2-1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles