31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tamisemi yatangaza majina ya madaktari 610 walioajiriwa

Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

OFISI ya Rais Tamisemi imetangaza ajira za kada ya afya daraja la pili kwa Madak- tari 610 watakao hudumu katika hospitali za Halmashauri mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa orodha hiyo inayopa- tikana kwenye tovuti rasmi ya Tamisemi Mkoa wa Arusha una jumla ya madaktari 26, Mkoa wa Tanga madaktari 33, Mkoa wa Kilimanjaro madaktari 10 na mkoa wa Manyara madaktari 18.

Kanda ya kati Mkoa wa Dodoma umepata jumla ya madaktari 31 huku Mkoa jirani wa Singida ukiwa na madak- tari 24

Nyanda za juu Kusini katika mkoa wa Iringa umepata madaktari 13, mkoa jirani wa Mbeya madaktari 33, mkoa wa Njombe Madaktari 19 na mkoa wa Song- we madaktari 17.

Upande wa mikoa ya Kanda ya Ziwa Mkoa wa Geita umepata madaktari 22, Mkoa wa Mwanza Madaktari 25, Mkoa wa Mara Madaktari 38 na Mkoa wa Kag- era ukiwa na madaktari 25.

Upande wa Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar es Salaam una madaktari nane, mkoa wa Pwani madaktari 35 na mkoa wa Morogoro madaktari 20.

Kanda ya Kusini mkoa wa Lindi una madaktari 28 na Mtwara madaktari 27. Mikoa mingine ni Kigoma madaktari 28, Simiyu madaktari 22, Ruvuma madaktari 24 na mkoa wa Rukwa madaktari 21.

Ajira hizo zinakuja ikiwa ni miezi mi-

tatu tu imepita tangu Februari 20, mwaka huu Rais Dk. John Magufuli alipotoa kibali cha ajira 1,000 za madaktari nchini.

Rais Magufuli alitoa kibali hicho kwa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inayoongo- zwa na Kapteni Mstaafu George Mku- chika kuajiri madaktari 1000.

Rais Magufuli alitoa kibali hicho al- ipohudhuria maadhimisho ya siku ya madaktari katika ukumbi wa mikutanao wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Ninafahamu kuna madaktari 2,700 bado hawajaajiriwa, nitalifanyia kazi” alisema Rais Magufuli na kuendelea kwa kumuuliza Waziri Mkuchika uwezekano wa kuajiri Madaktari 1000.

“Tuajiri madaktari 1000 na wasam- bazwe vizuri katika Mikoa yote” alisema Rais Magufuli, kauli ambayo ilipokelewa kwa furaha na shangwe kutoka kwa wa- jumbe waliohudhuria mkutano huo wa 55 wa Chama cha madaktari Tanzania (MAT).

Aidha, Rais Magufuli aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano im- ewekeza nguvu kubwa kwenye Sekta ya Afya nchini kwa kujenga miundombinu (majengo) pamoja na ununuzi wa vifaa tiba na mashine za kitaalam na kusema kuwa bila ya kuwa na wataalam wa ku- tosha bado Sekta ya Afya itakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa huduma bora za afya.

“Tuanze na madaktari 1,000, mambo yakiwa vizuri tena tutaajiri wengine, tu-

nahitaji madaktari mpaka vijijni, tume- jenga vituo vya afya 352 tumejenga Hos- pitali za Wilaya 77 zote hizi zinahitaji madaktari” alisema Rais Magufuli.

TAARIFA YA TAMISEMI

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Tami- semi iliyotolewa jana na Katibu wake mkuu, madtari hao wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa Mei 11-25, mwaka huu.

Kwamba watakaoshindwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kwa tarehe hizo bila ya taarifa nafasi zao zitajazwa haraka na waombaji wengine wenye sifa.

Aidha madaktari hao waliopangi- wa kazi wametakiwa kuwasilisha kwa waajiri wao ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa) vyeti halisi kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kupewa barua za ajira .

Vyeti ambavyo wanatakiwa kuwasili- sha ni pamoja na cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha nne na sita /Diploma, cheti cha kuhitimu shahada ya udaktari, cheti cha Usajili wa Baraza la Madaktari Tanzania (MCT) na uthibitisho wa ku- maliza mazoezi kwa vitendo (internship)

MAT

MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta Rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Elisha Osati kwa ajili ya kuzungumzia hatua hiyo ya Serikali lakini aliomba atafutwe baadaye kutokana na kuwa kwe- nye kikao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles