28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi wanandoa wanaodaiwa kusema hakuna corona kuanza kunguruma

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kuanza kusikiliza maelezo ya awali ya kesi inayowakabili wanandoa ambao wanadaiwa  walisema hakuna corona Juni 8.

Maelezo ya awali ya kesi hiyo yalipaswa kusomwa jana, lakini hakimu anayesikiliza kesi hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo alikuwa na udhuru.

 Washtakiwa ni Boniface  Mwita (49) mfanyabiashara  mkazi wa Tabata Kimanga na mkewe  Rosemary Jenera (41) ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kutoa matamshi hatarishi kwamba hakuna corona nchini.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, lakini hakimu anayeisikiliza ana udhuru.

Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 8, kwa ajili ya maelezo ya awali na washtakiwa wako nje kwa dhamana.

Awali Wakili  Wankyo akisaidiana na Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga walidai washtakiwa wanakabiliwa na kosa la kutoa lugha hatarishi ama yenye kushawishi jamii.

Walidaiwa Machi 20, mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam, wakiwa kwenye daladala la kutoka Tabata kuelekea Muhimbili lenye namba ya usajili T 119  DKS aina ya Toyota Coaster, walitoa matamshi hatarishi.

Walidai; ”Ugonjwa wa corona Serikali inadanganya, hakuna ugonjwa wowote na imefunga mashule kwa kuwa haina pesa na ada za kusomesha watoto bure.”

Hakimu Mwaikambo aliwaachia kwa dhamana washtakiwa baada ya kutimiza masharti ya kuwa na  wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho na kusaini bondi ya Sh milioni tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles