LILE bifu la kugombania jina la Simba ambalo linawahusisha wasanii nyota wa Bongo Fleva, Henry Samir ‘Mr Blue’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’ limemuibua mkongwe Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ ambaye alikuwa kwenye mishe za siasa.
Afande Sele maarufu Mfalme wa Rymes, aliyekuwa akigombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Mjini, amesema yeye ndiye mwanzilishi wa jina hilo miaka mingi iliyopita.
“Hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuambia, mimi ndiye Simba Dume. Mwaka 2008 nilifanya wimbo na P Funk Majani, unaitwa Simba Dume na nikaanza kutumia hilo kutokea hapo, nawashauri waachane na mabifu yasiyo na maana.
“Ni bora wote watatu tukutane, tufanye kolabo, kila mmoja aelezee usimba wake kwenye mashairi, naamini itabamba na itakuwa na maana na faida kwa kila mmoja na mashabiki wetu,” alidadavua Afande Sele.