26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 16, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kunoa makali Kombe la Mapinduzi

Kikosi-Yanga NA ZAINAB IDDY,  DAR ES SALAAM

TIMU ya Yanga tayari imewasili Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kesho huku wakitamba kutwaa ubingwa na kusaka makali kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Katika mashindano ya Mapinduzi, Yanga imepangwa kundi B ikiwa na Azam, Mtibwa Sugar na Mafunzo ya Zanzibar ambapo inatarajia kufungua dimba kesho kwa kuvaana na Mafunzo.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Hans Vans Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, tayari kipo visiwani Zanzibar.

Katika misimu ya hivi karibuni, Yanga wamekuwa wakilalamikiwa kutokana na kupeleka kikosi B lakini msimu huu wameamua kutuma kikosi kamili wakiwa na malengo ya kutwaa ubingwa pamoja na kuongeza ujuzi kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Akizungumza kabla ya kuelekea Zanzibar, kocha Pluijm alisema kutokana na ugumu wa kundi walilopo ana imani kubwa utatoa changamoto kwa wachezaji wake ambao bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanatetea ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Kikosi changu kamili kitakuwa Zanzibar na kila mchezaji atapangwa kulingana na uwezo wake atakaoonyesha kwenye mazoezi na baadhi ya mechi nimepanga kuwatumia wote kwani bado nina kazi kubwa mbele yangu.

“Nafikiri mashindano ya Mapinduzi yataongeza hali ya kimchezo kwa wachezaji wangu, kupitia mashindano hayo nitapata nafasi ya kuangalia mapungufu na kuyafanyia kazi na hii ni baada ya kukutana na timu ambazo hatujazizoea,” alisema.

Alisema baada ya Kombe la Mapinduzi kikosi chake kina kazi kubwa ya kujijenga ili kiweze kufanya vizuri katika kukabiliana na wapinzani wao, Cercle de Joachim ya Mauritius kwenye hatua ya kwanza ya mtoano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles