29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauji ya mwalimu

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

JESHI La Polisi mkoani Dodoma, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Mwalimu Eradius Lucas Mgaya wa Kijiji cha Chilungulu, Tarafa ya Bahi .

Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akiongea na waandishi wa habari.

Alisema tukio hilo  lilitokea Aprili 7, mwaka huu ambapo inadaiwa kuwa watuhumiwa hao watano (hakiwataja majina)walimpiga mwalimu huyo na kitu chenye ncha kali na kumtupa kwenye shamba la shule baada ya kumvizia njiani wakati akirejea nyumbani kwake .

“Bado tunaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la kifo cha Mwalimu Godfrey na tunaendelea kuwashikilia watuhumiwa wa mauaji hadi hapo uchunguzi utakapo kamilika,” alisema Kamanda Muroto.

Wakati huo huo Kamanda huyo wa Mkoa wa Dodoma aliwataka wenye magari kuchukua tahadhari kuhifadhi magari yao katika mazingira salama ikiwa ni pamoja na kuepuka kuegesha magari katika mazingira yanayowavutia wahalifu kuiba.

Alisema uchunguzi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa umebaini kuwa magari yanayowaniwa zaidi ni yale yanayotumia funguo za ‘Sensor’ ambazo hazihitaji kuchongwa .

“Tunawashauri kuchukua tahadhari zote ikibidi wafunge Car truck system kwenye magari au CCTV kamera kuongeza utambuzi wa wahalifu baada ya matukio,”alisisitiza.

Aliwataka wenye magari kuwa makini na waosha magari, mafundi wao, madereva wanaotumia kusafirisha au kusafiri nao safari za mbali .

“Wapo wageni wanaofika Dodoma kuazima magari kutembelea kwa matumizi binafsi kisha kuondoka ni vema kujua mienendo ya watu hao kwa sababu wanaweza kuwa chanzo cha kuandaa mazingira ya wizi wa magari,” alisema Muroto.

Pamoja na Mambo mengine Kamanda huyo wa Dodoma alisema jeshi hilo linamshikilia Grace Rauwo (31), mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ali jijini Dar es Salaam kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao.

Alieleza kuwa Rauwo akiwa na gari lenye namba za usajiri T 745 DSS aina ya Toyota Crown rangi nyeupe analolitumia katika uhalifu na linalodhaniwa kuwa ni la wizi ambapo anafanya uhalifu huo na timu ya wenzake wakiwa wanajihusisha na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao wakiwa wamejisajili Kama mawakala.

“Grace na wenzake wamechonga laine za simu wanaingilia mifumo ya neno Siri za wateja na kiwaibia fedha ambapo kabla ya kukamatwa waliiba fedha kwa njia ya mtandao Shilingi milioni 27 na kugawana huku yeye akiamua kununua gari hilo lenye namba za usajili Namba T.749 DSS ambalo pia wanalitumia kufanyia uhalifu,” alisema

Pamoja na halo pia alisema kuwa katika hatua lingine Jeshi hilo limemkamata Godfrey Shirima (22)  ambaye ni mpiga picha mkazi wa Mtaa wa Image Dodoma, akiwa na silaha aina ya bastola yenye namba za usajili 016975 akiimiliki kinyume na sheria ambapo amekuwa aikitumia katika matukio ya uhalifu.

Kwa mujibu wa Kamanda Muroto mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.

Aidha Kamanda huyo akitoa salamu za Sikukuu ya Pasaka alisema Jeshi la Polisi linategemea hakutakuwa na mikusanyiko isiyo ya lazima itakayoleta msongamano hasa wakati huu ambao kila raia anapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya COVID 19 .

“Wazazi wawalinde watoto wao na wasiwaruhusu kwenda kwenye mikusanyiko kama ilivyozoeleka, pia nawaomba watu wajiepushe na ulevi wa kupindukia na kuchukua tahadhali ya usalama barabarani,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles