27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mo Dewji atamba, Nchimbi akomaa

Zainab Iddy – Dar es Salaam

IKIWA imesalia siku moja kabla ya pambano la watani wa jadi, Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ amewahakikishia ushindi wapenzi na mashabiki klabu hiyo.

Simba itakuwa mgeni wa Yanga katika  pambano la mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, litakalopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zilipokutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja huo, matokeo yalikuwa sare ya 2-2.

Katika mchezo huo ambao Simba ilitangulia kufunga mabao mawili kabla ya Yanga ambayo ilikuwa mgeni kusawazisha.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, MO, aliandika maneno ya kumpongeza kocha Sven  Vandenbloeck kwa kukifanya kikosi cha Simba kucheza soka la kuvutia.

“Hongera kocha Sven kwa kazi nzuri, kwa kweli wachezaji wetu wanajituma kwenye michezo yote tunayocheza, hii ni kutokana na juhudi zako, sina shaka na mechi inayokuja ya watani wetu bila shaka pointi tatu zitakuwa zetu kuelekea safari ya  kutimiza malengo yetu ya ubingwa msimu huu.

“Siku zote mpira una matokeo matatu , lakini kwetu tunalikubali lile la kushinda ikitokea tumefungwa au sare itakuwa ni bahati mbaya,  ingawa najua haitokuwa kazi rahisi kwa watani zetu kutufunga, lazima tutimize kile tulichoshindwa kukifanya katika mechi ya mzunguko wa kwanza,”aliandika Mo.

Kauli hiyo ya MO inashabihiana na ile ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza ambaye ameweka wazi kuwa
ana uhakika wa kuvuna pointi tatu  na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao.

“Tayari nina uzoefu wa mechi za ‘derby’(Watani) hapa Tanzania, safari hii tumefanya maandalizi makubwa kuelekea mchezo na Yanga, mashabiki wasiwe na wasiwasi wajitokeze kuisapoti timu yetu kwa sababu  uhakika wa pointi tatu tunao kutokana na ubora wa kikosi chetu,”alisema Senzo.

Katika msimamo wa Ligi Kuu,  Simba inakamata usukani ikiwa na pointi 68, baada ya kucheza michezo 26, ikishinda 22, sare  mbili na kuchapwa mara mbili.

Mtani wake Yanga, yupo nafasi ya tatu akiwa na pointi 47, baada ya kushuka dimbani mara 24, akishinda michezo 13, sare nane na kuchapwa mara tatu.

Ssssssssssssssss

Nchimbi atamba kunasa kila kitu Simba
NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

IKIWA imesalia siku moja kabla ya pambano la watani wa jadi, straika wa Yanga,  Ditram Nchimbi amesema kikosi chao kitaingia  uwanjani kikiwa kinafahamu aina ya mpinzani wanayekutana  naye.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba, katika pambano la mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, litakalopigwa kesho, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo litakuwa la pili kwa Nchimbi likihusisha wapinzani wa jadi, baada ya lile la mzunguko wa kwanza lililopigwa Januari  mwaka huu na kumalizika kwa sare  ya mabao 2-2.

Fowadi huyo mwenye kasi na nguvu alitua Yanga, dirisha dogo la usajili, akitokea Polisi Tanzania, ambayo alikuwa akiitumikia kwa mkopo baada ya kutolewa na Azam. 

Akziungumza na MTANZANIA jana, Nchimbi alisema hawana presha na mchezo huo kwakua wamejiandaa kiasi cha kutosha kuekelea mpambano huo.

Alisema anawafahamu wachezaji wa timu pinzani wanayokutana nayo kutokana na kukutana nayo kwenye mazingira tofauti, ikiwemo Timu ya Taifa, nje ya uwanja na

 kuwafatilia kwa ukaribu.

“Tunatambua aina ya wachezaji ambao tunakwenda kukutana nao, tunajipanga kuona namna gani tutapata matokeo mazuri kwani na sisi tuna timu nzuri.

“Lengo letu ni kupata matokeo na tunajua nini mashabiki wetu wanahitaji kutoka kwetu,” alisema Nchimbi na kuongeza.

“Nawaomba mashabiki wetu wasiwe na hofu wajitokeze kwa wingi kuona namna gani tutapambana ili kupata matokeo chanya.”

Simba inakamata usukani ikiwa na pointi 68, baada ya kucheza michezo 26, ikishinda 22, sare  mbili na kuchapwa mara mbili.

Mtani wake Yanga, yupo nafasi ya tatu akiwa na pointi 47, baada ya kushuka dimbani mara 24, akishinda michezo 13, sare nane na kuchapwa mara tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles