33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Corona sasa yafika nchi 85 duniani

MWANDISHI WETU na MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA

KESI mpya za hadithi ya virusi vya corona ambavyo vilianzia mji ulio katikati ya China wa Wuhan mwishoni mwa mwezi Disemba zimekuwa zikiripotiwa kila siku duniani kote.

Zaidi ya watu 3,381 wamekufa duniani kote kwa virusi hivyo ambavyo vinafahamika kwa jina jingine la kitalaamu kama COVID-19, huku zaidi ya maambukizi 97,000  yakithibitishwa hadi kufikia jana katika nchi nyingi duniani, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Nchi nyingine tatu za Afrika ambazo ni Afrika Kusini, Cameroon na Senegal nazo zimeripoti visa vya kwanza vya maambukizi hayo na hivyo kufanya jumla ya nchi za Afrika zilizothibitisha kufikia sita.

Ifuatayo ni orodha ya nchi takribani 85 kati ya 195 (sawa na asilimia 44) duniani zilizothibitisha kesi za virusi vya corona hadi sasa:

Afghanistan – 1

Baada ya kuthibitisha kesi ya kwanza ya virusi vya corona Februari 24, Wizara ya Afya ilitangaza hali ya dharura katika jimbo la magharibi la Herat, ambalo linapakana na Iran.

Algeria – 17

Andorra – 1

Argentina – 1

Armenia – 1

Australia – 52

Austria – 29

Azerbaijan – 3

Bahrain – 52

Belarus – 6

Ubelgiji – 23

Bosnia – 2

Brazili – 4

Serikali ya Brazili ilithibitisha maambukizi ya virusi hivyo kwa mara ya kwanza Februari 26 baada ya kifo cha  mwanaume mwenye miaka 61 ambaye alitembelea Italia mwezi huo huo  na hivyo kuwa nchi ya kwanza la Latini Amerika  kuthibitisha kesi ya virusi hivyo.

Mwanaume huyo wa Brazil inaelezwa kabla mauti hayajamkuta alitumia wiki mbili  kaskazini mwa Italia huko Lombardy alikokuwa kikazi na inaelezwa kuwa aliambukizwa virusi hivyo akiwa huko, wizara ya afya inasema.

Cambodia – 1

Cameroon – 1

Kesi ya kwanza ya virusi vya corona iliripotiwa Cameroon jana, Machi 6 mwaka huu.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, mgonjwa mwenye umri wa miaka 58 ambaye ni raia wa Ufaransa, aliwasili mjini Yaounde Februari 24.

Canada – 34

China – 80,710

Hadi kufikia jana Machi 6, jumla ya watu waliothibitika kuambukizwa virusi hivyo nchini China walikuwa jumla 80,710, wengi wao wakiwa kutoka jimbo la Hubei. Takribani watu 3,042  wamekufa, kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Afya ya nchini China.

Eneo la Macau limethibitisha kesi 10 , wakati  Hong Kong walioathirika wakifika 100.

Croatia – 10

Jamuhuri ya Chile – 8

Denmark – 10

Jamuhuri ya Dominica – 1

Ecuador – 10

Misri – 3

Wizara ya afya ya Misri iliripoti kisa cha kwanza cha virusi hivyo Februari 14 na hivyo kuandika rekodi ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika.

Maofisa wanasema mtu huyo wa kwanza kuthibitika kuwa na virusi hivyo nchini humo alikuwa ni raia wa kigeni na Februari 19, WHO ilisema aliruhusiwa kutoka hospitali.

Estonia – 2

Finland – 7

Ufaransa – 285

Georgia – 3

Ujerumani – 534

Ugiriki – 10

Hungary – 2

Iceland – 26

India – 31

Indonesia – 2

Iran – 3,513

Takribani watu 77  wamethibitishwa kufariki kwa ugonjwa huo nchini Iran hadi kufikia Machi 4,  kwa mujibu wa WHO.

Wakati huo huo watu walioathirika na virusi hivyo wakiongezeka hadi kufikia 2,922.

Miongoni mwa watu maarufu aliyethibitika kupata virusi vya corona ni Masoumeh Ebtekar, ambaye ni makamu wa rais wa wanawake nchini Iran.

Iraq – 36

Iraq ilitangaza kifo cha kwanza kilichotokana na virusi hivyo Machi 4 mwaka huu.

Mwanaume mwenye umri wa miaka 70 alifariki dunia katika jiji la Sulaimaniyah,  kaskazini mwa  Iraq

Ireland – 6

Israel – 15

Italia – 3,089

Hadi kufikia Machi 3, idadi ya watu walioathirika ilisimamia 2,502, wengi wao wakiwa ni kutoka eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo huku jumla ya waliokufa wakiwa 79.

Japan – 331 na 706

Jumla ya watu  705 waliookolewa nchini China ambao waliokuwa wamewekwa karantini kwenye meli ya Diamond Princess ambayo ilitia nanga Yokohama walithibitika kupata maambukizi ya virusi hivyo Februari 27.watu wazima wanne waliokuwamo katika meli hiyo walifariki dunia.

Kwa mwongozo wa WHO, Japan haijumlishi idadi ya watu waliokuwamo kwenye meli hiyo katika idadi ya kitaifa ya walioathirika na virusi hivyo

Takwimu za kitaifa zinaonyesha jumla ya walioambukizwa virusi hivyo nchini humo ni 331  hadi kufikia Machi 4, vikiwamo vifo 12.

Jordan – 1

Kuwait – 56

Latvia – 1

Lebanon – 13

Kisa ya kwanza cha virusi vya corona kilithibitishwa Lebanon Februari 21  baada ya mwanamke wa Iran kuingia nchini humo na alipopimwa alionekana kuwa na maambukizi.

Lithuania – 1

Luxembourg – 1

Malaysia – 50

Mkurugenzi Mkuu wa Afya wa Malaysia, Noor Hisham Abdullah  alisema watu 22 walioathirika wameruhusiwa kutoka hospitali.

Mexico – 5

Monaco – 1

Morocco – 1

Nepal – 1

Netherland – 82

New Zealand – 3

Nigeria – 1

Nigeria ilithibitisha kisa cha kwanza baada ya raia wa Italia anayefanya kazi Lagos kutembelea to Milan  mwezi uliopita, Februari February 28. Maofisa wa afya wanasema mtu huyo alikuwa Nigeria  kwa siku mbili kabla ya kutengwa,  na hivyo kuipa kazi mamlaka ya kuwatafuta watu wengine aliokaribiana nao.

Mtu huyo anakuwa wa kwanza kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo katika eneo la Jangwa la Sahara.

North Macedonia – 1

Norway – 56

Oman – 15

Pakistan – 6

Ufilipino – 5

Poland – 1

Ureno – 5

Qatar – 8

Romania – 4

Urusi  – 5

San Marino – 16

Saudi Arabia – 2

Wizara ya afya ya Saudi Arabia ilitangaza kisa cha kwanza Machi 3 mwaka huu.

Muathirika huyo alitembelea Iran, Bahrain, eneo linaloongozwa na Saudia.

Senegal – 4

Singapore – 110

Slovenia – 1

Afrika Kusini – 1

Korea Kusini – 6,593

Nje ya China, nchi ya Korea Kusini ndiyo yenye idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona. Watu 26  wamekufa baada ya kupata virusi hivyo.

Hispania – 222

Sri Lanka – 1

Sweden – 52

Uswisi- 90

Taiwan – 42

Taiwan imethibitisha kesi 41, ikiwamo ya mwanaume mwenye umri wa miaka 61 ambaye mbali na kuwa na matatizo mengine ya kiafya alifariki kwa virusi hivyo.

Thailand – 47

Tunisia – 1

Ukraine – 1

United Arab Emirates – 28

Februari 1, UAE ilikuwa nchi ya kwanza Mashariki ya Kati kuthibitisha kesi ya virusi vya corona.

Uingereza – 90

Marekani – 148

Kesi za Marekani ni pamoja wale waliokuwamo katika meli ya Diamond Princess iliyokuwa imetia nanga nchini Japan.

Ukraine – 1

Kisa cha kwanza cha virusi vya corona kilithibitishwa Ukraine Machi 3  baada ya mwanaume mmoja aliyetoka Italia akipitia Romania vipimo vyake kuonyesha ameathirika.

Vatican – 1

Vatican iliripoti mgonjwa huyo  jana Machi 6,

Vietnam – 16

Februari 13,  wizara ya afya ilithibitisha kisa cha 16 cha corona. Watu hao wote 16 wanaendelea vizuri kwa mujibu wa mamlaka za afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles