32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy: Wanaume mnaopigwa na wake zenu toeni taarifa madawati ya jinsia

Simiyu 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema anatambua kuwa kuna baadhi ya wanaume wanapata vipigo kutoka kwa waume zao na kuwataka wajitokeze ili wapate msaada.

Aliyasema hayo jana wakati akifungua maonesho ya wanawake wajasiriamali na kuupokea msafara wa kijinsia ambao unazunguka katika mikoa tisa kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Alisema anazo taarifa za wanaume wanaopata vipigo kutoka kwa wenza wao na kuwataka wasione aibu kutoa taarifa kwenye madawati ya jinsia ili wapate msaada. 

“Ingawa unyanyasaji wa vipigo uko kwa wanawake lakini wanaume msiogope kuripoti pale mnaponyanyaswa ili mpate msaada,” alisema.

Ummy alifungua maonyesho hayo ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi nane.

Aidha alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, John Jingu kwa kufanikisha  maadhimisho  hayo zikiwemo taasisi mbalimbali.

Akizungumzia uboreshaji wa bidhaa lishe alisema Wizara ya Kilimo na Wizara ya  Afya, zinaweza kushirikiana kuboresha chakula lishe kwa watoto ili kukabiliana na udumavu kwa watoto.

Aliongeza huduma na elimu kupitia misafara ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoratibiwa  na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

“Misafara hii imewafikia watu wengi na kupata elimu itakayowasaidia kuondokana na  vitendo vya ukatili,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu, alisema wizara kwa kushirikiana na wadau imejidhatiti kuhakikisha inatoa elimu kwa jamii ili kuweza kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema wizara yake inatambua mchango wa wanawake katika sekta hiyo. 

“Kila penye wakulima wanne, watatu ni wanawake hivyo mchango wa wanawake katika kilimo ni mkubwa tunautambua sana mchango wenu wanawake,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles