31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Samia awatwisha mzigo wananchi ulinzi chuo cha IFM

Derick Milton – Simiyu

MAKAMU wa Rais Samia Suruhu Hassan, amewataka wananchi wa Kijiji cha Sapiwi Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, kunakojengwa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuwa walinzi wa chuo hicho.

Alisema Serikali inalo jukumu la kukisimamia chuo hicho, lakini jukumu la ulinzi na wa mali za chuo na wanafunzi upo mikononi mwa wananchi.

Alitoa wito huo jana, wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa majengo manne ya chuo hicho tawi la Simiyu.

 “ Matunzo na ulinzi wa chuo hiki na mali zake, vyote vinawategemea nyie wananchi, sisi Serikali kazi yetu ni kuendesha chuo, lakini ulinzi uko mikononi mwenu, nawaomba wananchi kuweni walinzi na mkitunze chuo hiki,” alisema Samia.

Alisema uwepo wa chuo hicho katika kijiji hicho utasaidia kukuza uchumi wa wananchi mmoja kwa mmoja, ikiwa ni pamoja na kukua kwa uchumi wa kijiji hicho na wilaya kwa ujumla.

Aidha alisema Serikali itachimba kisima kikubwa cha maji kwa ajili ya kuwahudumia wananchi walioko karibu na chuo hicho ikiwa na kuwaletea huduma ya umeme.

Awali akiongea kwenye hafla hiyo Naibu Waziri wa Fedha Ashatu Kijaji, aliutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kinazalisha wanafunzi wenye hofu ya Mungu, uzalendo na uhadilifu.

Alisema Wizara yake imekiagiza chuo hicho kuongeza somo la maadili na usimamizi wa fedha, ili wanafunzi watakao kuwa wanahitimu waweze kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.

Aidha alizitaka taasisi zote za fedha nchini, kutumia fursa ya uwepo wa chuo hicho, kuhakikisha wanasogeza huduma za kifedha karibu kwa ajili ya wanafunzi.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Thadeo Satta, alisema ujenzi wa chuo hicho utakamilika Mei 2020, ambapo kwa awamu ya kwanza watadahili wanafunzi 1,000.

Alisema udahili huo wa wanafunzi utaanza kufanyika Septemba ambapo wataanza na wanafunzi wanaochukua masomo ngazi ya cheti.

Profesa Satta alisema ujenzi wa awamu ya kwanza wa chuo hicho unagharimu Sh bilioni tatu ambapo utahusisha nyumba sita za wafanyakazi, ukumbi wa mikutano, vyumba vinne vya madarasa, mabweni ya wanafunzi na mgahawa wa chuo.

Alisema huduma hiyo ya kwanza inahusisha pia, maktaba yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 120 kwa wakati mmoja, maabara ya kompyuta yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 120.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles