30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Wenye matatizo ya moyo 200 wawekewa betri JKCI

Aveline Kitomary – Dar es Salaam

MKURUGENZI wa tiba ya moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Peter Kisenge, amesema kwa kipindi cha mwaka jana wagonjwa 200 wenye matatizo ya umeme wa moyo wamewekewa betri (Pacemaker).

 Akizungumza wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyofanyika jana katika taasisi hiyo, Dk Kisenge alisema watawawekea wagonjwa wawili betri hizo.

“Siku ya leo katika taasisi hii tumefanya kambi maalum ya kuwahudumia wagonjwa 14 wenye matatizo ya umeme wa moyo na mishipa iliyoziba.

“Tutawawekea betri wagonjwa wawili wenye matatizo ya mapigo ya moyo kuwa chini ya 40 na walikuwa wanapata matatizo wanapofanya shughuli zao wakati mwingine wanaanguka  kwasababu mapigo ya moyo yako chini,”alibainisha Dk Kisenge.

Alisema wagonjwa 10 watapatiwa huduma ya kuzibua mishipa ya moyo na kuweka vifaa maalum vinavyoitwa vizibua njia  ili waweze kuendelea na kazi zao.

Dk Kisenge ambaye pia ni Daktari bingwa moyo alisema magonjwa ya moyo yanaongezeka kwa kasi hivyo uwepo wa taasisi hiyo umeokoa kiasi cha Sh bilioni 25 za matibabu ya nje ya nchi.

“Tunaweka betri za aina mbalimbali ambapo tunaita low power device na high power deice hizi sisi tunaweza kuweka lakini bado nchi nyingine za Afrika hawajaweza kuweka.

“Tatatizo la umeme wa moyo ni pale mgonjwa anapokuwa na mapigo ya moyo ya juu au chini, mapigo  husaidia moyo kusukuma damu na kupeleka oksijeni sehemu mbalimbali za mwili hivyo mtu anapokuwa na tatizo moyo unashindwa kufanya kazi yake,”alieleza.

Akiainisha sababu za magonjwa ya moyo, alisema ni pamoja na ulaji wa mafuta yatokanayo na wanyama.

 “Sababu zingine ni umri mkubwa ambao unaweza kupunguza ufanyaji kazi wa moyo, kula vyakula vya wanga, unene uliokithiri, unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara,” alisema.

Alisema kwa magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo matataizo yanaanzi miaka  55 na wagonjwa wengi walionao ni kuanzia miaka 70 na kuendelea.

Alisema watu inabidi wabadili hali ya maisha na kwa kula vyakula bora na kufanya mazoezi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles