32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani wa ACT wahamia CCM

Andrew Msechu -Dar es Salaam

MADIWANI watano wa chama cha ACT Wazalendo mkoani Kigoma wametangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Walitangaza uamuzi huo jana katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.

Walisema wamechukua uamuzi huo kwa kujiuzulu nafasi zao za udiwani na nafasi zote za uongozi ndani ya ACT Wazalendo na kujinga na CCM kuanzia jana.

Madiwani hao ni Hamis Rashid (Kata ya Gungu), Amduni Nassor (Kata ya Kasingirima), Fuad Sefu (Kata ya Kasimbu), Ismail Hussein (Kata ya Kagera) na Mussa Ngogolwa (Kata ya Kipampa), wote kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akiwapokea madiwani hao, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alisema anafurahi kwa kuwa kila wanapopata mwanachama mpya uwezo wa chama katika kupambana na kuendelea kuongoza nchi na Serikali zake mbili unaongezeka.

Mmoja wa wanachama hao wapya wa CCM, Rashid alisema yeye pamoja na wenzake wameamua kuachia nafasi zao kama njia ya kukubali utendaji wa Serikali inayoongozwa na CCM.

“Sisi wote tulikuwa madiwani na tumekuja kueleza uhalisia wa kile kilichopo kwenye nafsi zetu. Kwa kifupi tunahama kuja kwenye chama kipya kuunga mkono juhudi ambazo kila mmoja ameshuhudia.

“Tuliridhia kwa nafsi zetu wenyewe na kukubaliana kuwa ili tuweze kushiriki katika kupeleka mbele mustakabali wa nchi yetu na kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa pamoja,” alisema Rashid.

Naye Nassor alisema amerudi nyumbani na hakuna cha kushangaza kwa kuwa kila mtu anaona, kwa hiyo amerudi CCM kwa kuwa kumenoga na anafurahishwa na sera za mwenyekiti wa CCM.

Sefu alisema bila kushawishiwa na mtu yeyote ameamua kujivua nyadhifa zote alizokuwa nazo ACT Wazalendo kwakuwa haoni sababu ya kuendelea kuwepo upinzani.

Hussein alisema ameamua kwa hiyari yake kuomba fursa ya kujiunga na CCM kwa kuwa anaona ndicho chama pekee chenye nguvu na kinachoweza kubadilisha nchi, kikijipambanua kwamba kinaweza kuibadilisha nchi na kuleta maendeleo.

Naye Ngogolwa alisema ameamua kuhamia CCM kwa kuwa ni chama kinachotoa fursa kwa vijana na kuwapa nafasi kubwa ya utumishi na kwamba atapambana kwa nguvu zake zote kuhakikisha CCM inaendeela kushika dola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles