Omary Mlekwa -Hai
MFANYABIASHARA wa wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni mkazi wa Bomang’ombe, Ramadhani Tesha (44), amefikishwa katika Mahakama yaHakimu Mfawidhi ya Wilaya hiyo akikabiliwa na shitaka la kumlawati mtoto wake mwenye umri wa miaka sita.
Akisoma hati ya mashitaka, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Lobulu Mbise, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Devota Msofe, alidaiwa mshitakiwa anakabiliwa na shitaka la kumlati mtoto wake anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kingereka wilayani humo uku akitambua kufanya hivyo ni kosa.
Mbise alidai Januar 23 mwaka kwa nyakati tofauti katika eneo la Kibaoni Bomang’ombe, mtuhumiwa alimfanyia ukatili huo mtoto wake kinyume na kifungu 154 (11) (a) (2) cha sheria ya adhabu sura 16 kama iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka lake na mahakama kushindwa kutoa dhamana kwa mshitakiwa kwa kohofia usalama wake kutokana na jamii inayomzunguka kuhofiwa kumdhuru kutokana na na tukio hilo.
“Kesi hii ninaiharisha hadi Februari 13 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na mtuhumiwa utakwenda magereza hadi hiyo siku kutokana na hali ya usalama wako kwenye jamii” alisema hakimu.