27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Morrison awaka tena Yanga ikitinga 16 bora

Winfrida Mtoi-Dar es Salaam

TIMU ya Yanga imeifuata Simba hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho(ASFC), baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons,katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba ilifuzu 16 bora ya michuano hiyo, baada ya juzi kuitungua Mwadui mabao 2-1, mchezo uliopigwa pia kwenye uwanja huo.

Yanga baada ya kutinga hatua hiyo, sasa itakutana na timu daraja la kwanza ya Gwambina, ambayo juzi iliifurusha mashindanoni Ruvu Shooting, kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 7-6, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga na Prisons jana ziliuanza mchezo kwa kasi huku kila moja ikionekana kupania kusaka ushindi na kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Dakika ya tisa, Adilly Buha alikuwa katika nafasi ya kuifungia Prisons bao la kuongoza lakini mkwaju wake ulikuwa laini kwa kipa wa Yanga,Metacha Mnata

Dakika 11,winga wa kimataifa wa Ghana, Benard Morrison aliifungia Yanga bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti baada ya mmoja wa mabeki wa Tanzania Prisons kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

David Molinga alipokea krosi safi ya Kaseke, lakini akashindwa kuukwamisha mpira wavuni.

Dakika ya 36,Ezekia Mwashilindi alijaribu kumtungua Metacha lakini kiki yake ilitoka nje ya lango la  Yanga.

Dakika ya 41, Prisons ilifanya shambulizi kali langoni mwa Yanga, lakini kiki ya Salum Kimenya ilipaa.

Kipindi cha kwanza kilikamilika kwa Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili, kilipoanza Prisons iliingia uwanjani na nguvu zaidi ikikusudia kusawazisha.

Dakika ya 53, Ismail Aziz alimtengenezea pasiJeremia Juma ambaye alikosa utulivu baada ya fataki lake kutoka nje ya lango la Yanga.

Dakika 62, mwamuzi wa mchezo huo, Athuman Lazi alimlima Kimenya kadi ya njano, baada ya kumkwatua Haruna Niyonzima wa Yanga.

Dakika ya 64, Yikpe aliifungia Yanga bao la pili kwa kichwa baada ya kupokea pasi ndefu ya Morrison.

Kipa wa Prisons Jeremiah Kisubi alionyesha umahiri dakika ya
74, baada ya kudaka kiki ya Morrison.

Dakika ya 79, beki Juma Abdul alionyeshwa kadi ya njano, baada ya kumkwatua Mwashilindi.

Kila upande uliendelea kufanya mashambulizi ili kusaka mabao, Yanga ikitaka kuongeza wakati Prisons ikisaka kufunga la kwanza na kusawazisha kabla ya kuongeza mengine.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga,  Luc Eymael, alisema amefurahishwa na matokeo ya kikosi chake sambamba na kiwango walichokionyesha wachezaji wake.

“Tumecheza vizuri na tumefanikiwa kupata ushindi ambao ndiyo kitu muhimu zaidi kwetu,”alisema Eymael.

Kikosi cha Yanga

Metacha Mnata,Juma Abdul,Jaffar Mohammed, Lamine Moro,Abdul Azizi Makame, Deus Kaseke/ Patrick sibomana( dk 81), Haruna Niyonzima, David Molinga/ Yikpe Gislain(dk 57), Mapinduzi Balama, Benard Morrison/ kuingia Feisal Salum/(dk).

Kikosi Cha Prisons

Jeremia Kisubi, Michael Ismail, Benjamin Asukile, Vedastus Mwigambi, Nurdin Chana, Adilly Buha,Salum Kimenya/ Samson Mbangula (dk 67), Ezekia Mwashilindi, Jeremia Juma/ hamidi Mohammed (89),Paul Peter, Azizi Ismail/ Cleophace Mkandala (dk 80).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles