27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yajipanga kukabili tatizo la ajira nchini

Tunu Nassor – Dar es Salaam

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kutatua tatizo la ajira nchini ambalo linazidi kuongezeka.

Akizungumza juzi katika shindano la wajasiriamali wanavyuo la Global Student Entrepreneur Award (GSEA), Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde alisema wanafarijika kuona kuna taasisi zimeanza kulifanyia kazi tatizo hilo.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa tatizo bado ni kubwa hivyo njia pekee ya kupunguza tatizo hilo ni kushirikiana na sekta binafsi katika kuwajengea uwezo vijana kuzalisha ajira.

“Tumefarijika kuona taasisi zinajitokeza kuwasaidia kuwajengea uwezo vijana kuweza kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine hivyo kama serikali tutashirikiana nao kuhakikisha wanatimiza lengo hilo,” alisema Mavunde.

Alisema nchi inatakiwa kuwawezesha vijana wake kwa kuwajengea miundombinu wezeshi waweze kujiajiri.

“Tutaendelea kuwasaidia vijana kupata mitaji itakayowawezesha kuanzisha biashara zao waweze kuwasaidia wengine wasio na ajira,” alisema Mavunde.

Aliongeza kuwa wanaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili vijana zikiwamo kutokuaminiwa na taasisi za fedha na kukosa mitaji.

Kwa upande wake, Msimamizi wa GSEA nchini, Baraka Mtunga alisema mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi 27 waliopo katika vyuo nane.

Alisema moja ya kigezo cha kuwa mwanachuo mjasiriamali bora ni kuwa na uwezo wa kuzalisha si chini ya Sh milioni moja kwa kipindi cha mwaka mmoja.

“Mshindi wa shindano hili amepata sh milioni moja na kupata msaada wa kibiashara chini ya taasisi ya Enterprenuers’ organization na kufanikiwa kushiriki katika mashindano ya Dunia  nchini Marekani,” alisema Mtunga.

Naye mshindi wa shindano hilo Mosses Katala alisema changamoto kubwa zinazosababisha  wanavyuo kushindwa kuanzisha biashara zao ni kukosa mitaji.

“Binafsi kwa kushirikiana na wenzangu ilibidi kuomba msaada wa kupata mtaji kutoka nje ya nchi ndipo tulipoanzisha utengeneaji wa chakula cha mifugo kupitia funza,” alisema Mosses.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles