31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Kivuli aitaka Serikali kuwekeza kwenye elimu

Ramadhan Hassan – Dodoma

WAZIRI kivuli wa elimu Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Suzan Lyimo ameitaka Serikali  kuwekeza zaidi katika elimu kwani ndiyo nyenzo kuu ya mabadiliko chanya ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dodoma, Lyimo  alisema kuwa suala la elimu ni la Kikatiba hivyo ni lazima msingi huo uzingatiwe kwa masilahi ya nchi.

“Miaka ya 1960 nchi kama Malaysia, Singapore na Thailand zilikuwa sawa na Tanzania lakini kwa kuwa waliwekeza kwenye sekta ya elimu zimepiga hatua kubwa, hivyo hata nchi yetu pamoja na mafanikio machache ingewekeza kwenye sekta hiyo ingepiga hatua kubwa kimaendeleo,” alisema

Alisema kuwa Seriakali imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha watoto wanaenda shule jambo ambalo sio halali na liko kinyume na utaratibu wa kisheria kwa sababu watoto wengine wanakosa elimu toshelevu.

“Jambo lingine ni kuwa walimu watapaswa kufundisha kwa muda wa ziada ili hali hawapati nyongeza ya mshahara wala motisha yoyote na ndiyo sababu inayoyushusha viwango vya ufaulu kwa shule za Serikali ukilinganisha na shule binafsi.

“Kila darasa linatakiwa kuwa na watoto 50 lakini kuna shule zina watoto mpaka 100 huku baadhi ya shule zikiwa na walimu wachache mambo ambayo pia yanachangia matokeo mabaya.

“Kwa hiyo niseme tu kwamba kuna tatizo kubwa la elimu  kwa sababu ya msongamano lakini pia Serikali kutokuwa na mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa wanajenga miundombinu ya madarasa hivyo ni vema kila Mwaka wakatenga fedha ya kutosha,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles